Tuesday, 3 May 2016

MKANDARASI WA KAMPUNI YA JASCO MKOANI GEITA ALALAMIKIWA NA WANANCHI WA MTAA WA JIMBONI KATA YA KALANGALALA


Wananchi wa mtaa wa Jimboni katika kata ya Kalangalala mkoani hapa wamemlalamikia mkandarasi wa Jasco kwa kushindwa kumaliza ujenzi wa barabara hali ambayo imesababisha  maji mengi kujaa katika maeneo yao na kusababisha mafuriko.

wakizungumza na Storm habari wananchi hao walisema kuwa  usiku wa kuamikia siku ya leo ambapo mvua imenyesha kwa muda mrefu imesababisha athari za maji mengi kuingia maeneo wanayoishi kutokana na kukosekana kwa mitaro  katika barabara hiyo.

Walitaja hasara walizozipata ni pamoja na vitu vingi hususani  vya umeme kuharibika pamoja na kushindwa kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa kutokana na namna na jinsi hali ilivyokuwa siku ya leo.


Aidha Storm habari ilifanikiwa kumpata mkandarasi wa kampuni hiyo,Bw.Maulid Abdalla,amesema kuwa  tatizo hilo wameliona na kwasasa wanalishughulikia na wamekwisha kuagiza watu waende kuchimba mitaro katika maeneo ambayo kumetokewa na tatizo.

No comments:

Post a Comment