Mifuko ya plastiki
inayofungasha pombe maarufu kama ‘viroba’ imepigwa marufuku na Serikali kuanzia
mwakani.
Sambamba na hilo Serikali pia, imepiga marufuku moja kwa moja utengenezaji, usambazaji, uingizaji nchini wa mifuko ya plastiki kuanzia mwaka huo.
Sambamba na hilo Serikali pia, imepiga marufuku moja kwa moja utengenezaji, usambazaji, uingizaji nchini wa mifuko ya plastiki kuanzia mwaka huo.
Waziri wa Nchi , Ofisi
ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba aliwaambia
wanahabari jana sehemu kubwa ya mifuko hiyo inayotolewa bure imekuwa ikichangia
uchafuzi wa mazingira kwa kiasi kikubwa.
Wakati Makamba
akiyasema hayo, Februari mwaka huu Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina aliondoa zuio la matumizi ya mifuko ya
plastiki akisema kuwa itaziweka rehani ajira za Watanzania wanaofanya kazi
kwenye viwanda vinavyotengeneza mifuko hiyo.
Pia, Mpina alisema
itapunguza kasi ya uwekezaji wa viwanda vilivyowekeza katika bidhaa hiyo.
Akizungumza katika
siku ya Mazingira Afrika, Mkurugenzi wa Mazingira, Dk Julius Ningu alisema
maamuzi hayo yamelenga kulinda viwanda vilivyoajiri mamia ya Watanzania, tofauti
na nchi nyingine zinazotegemea wazalishaji wa nje ya nchi.
Makamba akizungumzia
uamuzi mpya wa kuzuia mifuko ya plastiki, alisema matumizi ya mifuko
inayofungashia vileo na inayotumika katika matumizi mengine husambaa na
kuchafua mazingira. Alisema mifuko ya plastiki inatajwa kuziba mifereji na
kusababisha mafuriko na athari nyingine za mazingira.
“Leo (Jana), tumeamua kutangaza ili kuwaanda
wahusika wasiendelee kuwekeza katika mifuko hii badala yake wasubiri utaratibu
mwingine utakaowekwa na Serikali,” alisema Makamba na
kuongeza kuwa:
“Asilimia kubwa ya uchafu kwenye nyanzo
vya maji, mito, maziwa na fukwe za bahari ni mifuko ya plastiki.”
Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, alisema Serikali inakamilisha majadiliano ya ndani na baadaye itawahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku ya moja kwa moja mifuko hiyo.
Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, alisema Serikali inakamilisha majadiliano ya ndani na baadaye itawahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku ya moja kwa moja mifuko hiyo.
Alifafanua kwamba
Serikali itatoa muda kwa walioajiriwa, kujiajiri na kuwekeza kwenye biashara ya
mifuko hiyo ili kujiandaa kuacha shughuli hizo na badala yake itawezesha mazingira
ya utengenezaji na upatikanaji wa vifungashio mbadala.
“Kwa wanaotengeza mifuko hii na kuiuza katika soko la nje hatuna tatizo
nao waendelee. Ila kwa soko la ndani hawataruhusiwa kufanya hivyo.Zuio hili
litakuwa la kisheria siyo kwa maneno,” alisisitiza Makamba.
Aliongeza kuwa katika kuonyesha Serikali imedhamiria kupambana na hali hiyo wizara yake imeamua kutuma timu ya watu watano kwenda Rwanda kujifunza namna bora ya kudhibiti matumizi na kuzuia mifuko hiyo tangu mwaka 2008.

Waziri huyo alitoa
wito kwa watengenezaji, wasambazaji na waagizaji wa mifuko hiyo kujiandaa na
zuio hilo na katika siku zijazo Serikali itatoa utaratibu na maelekezo ya
tarehe ya kuanza zuio huku taratibu nyingine za kina zikifuata ili kuondoa
mkanganyiko.
Katika hatua
nyingine, Makamba alisema maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Mazingira Duniani
ambayo hufanyika Juni 5 kila mwaka hayatafanyika kitaifa badala yake wizara
imewaelekeza wakuu wa mikoa kufanya maadhimisho katika maeneo yao.
“Tumewapa miongozo kuhusu utekezezaji wa
shughuli hizo za maadhimisho zinazolenga kutoa hamasa ya hifadhi ya mazingira
hususan nyanzo ya maji amabayo ni muhimu kwa viumbe hai,” alisema Makamba.
Kwa mujibu wa Makamba,
kauli mbiu ya mwaka huu kitaifa juu ya maadhimisho hayo ni ‘ tuhifadhi vyanzo
vya maji kwa uhai wa taifa letu’aliwashauri na kuwataka Watanzania kutumia siku
hiyo kupanda miti, kudhibiti uchomaji wa misitu
Ofisa Mwandamizi Mazingira wa Nemc, Arnold Kisagala alisema nusu ya mifuko ya plastiki nchini inazalishwa na kuingizwa kutoka nchi jirani ya Kenya.
Ofisa Mwandamizi Mazingira wa Nemc, Arnold Kisagala alisema nusu ya mifuko ya plastiki nchini inazalishwa na kuingizwa kutoka nchi jirani ya Kenya.
Alisema agizo la
Waziri Makamba litawezekana, lakini linahitaji ushirikiano kutoka kwenye sekta
zingine kwa kuwa viwanda vingi vya mifuko ya plastiki vipo Kenya.
"NEMC tayari tulishaanza mazungumzo na
wazalishaji kuhusu mifuko ya plastiki,” alisema.
No comments:
Post a Comment