Katika kuhakikisha
mikoa ya Simiyu, Katavi, Geita, Njombe na Songwe inaondokana na matatizo ya
miundombinu serikali imeombwa kuipa kipaumbele cha bajeti mikoa hiyo ili kuweza kutatua
chanagamoto hiyo.
Akiuliza swali la
nyongeza katika kipindi cha maswali na majibu bungeni dk. Raphaeli Masunga
mbunge wa Busega ambapo amesema, je
serikali haioni kuwa kuna haja sasa kwa mikoa mipya na wilaya zingine kupewa
kipaumbele cha bajeti ili zipate mafungu ya kutosha.
Akijibu swali hilo
naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano mhandisi Edwini Ngonyani
amezitaka bodi ya barabara nchini pamoja na Tanroads kuzingatia mahitaji
mahususi yaliyoko katika mikoa hiyo pamoja na mikoa mingine ambayo ina
mazingira magumu ya usafiri.
Hata hivyo
mhandisi Ngonyani amesema
kuwa hadi kufikia june 2016 fedha zote za mfuko wa barabara zilizopangwa
kugharamia kazi za matengenezo na ukarabati wa barabara zitakuwa zimepokelewa
na kupelekwa kwa mawakala wa barabara.
No comments:
Post a Comment