Imebainika kuwa jamii kubwa inayoishi karibu na
Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM),
hususani maeneo ya vijijini bado hawajawa
na uelewa wa kutosha juu ya faida ambazo
zinatolewa na mgodi huo, ambao umekuwa ukishirikiana
na Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali huku wananchi wakiaminishwa kuwa hakuna faida
yoyote inayotokana na mgodi huo.
Kutokana na kuwepo kwa mawazo hayo GGM kwa
kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya
Geita wamefanya semina
kwa wanafunzi wa shule za sekondari huku lengo ikiwa ni kuwajengea
uelewa kuhusiana na Mgodi huo ili wawe mabalozi wazuri katika jamii inayouzunguka mgodi huo.
Kufuatia Semina hiyo Wanafunzi wamejifunza mambo mbalimbali, huku wakipata fursa ya kuuliza
maswali ambayo yalikuwa yakiwasumbua
kwa muda mrefu na miongoni mwa
mambo waliyoyauliza ni pamoja na suala la ajira Mgodini ambapo Meneja Mahusiano wa Mgodi Joseph Mangilima na Afisa
utamaduni wa halmashauri ya Wilaya ya Geita Bw.Mfungo Phares wakawa na
majibu
Meneja mahusiano wa GGM, Joseph Mangilima amesema
kuwa katika semina hiyo kuna maombi ambayo
yameombwa na wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuombwa kujenga mabweni kwa
shule zilizopo vijijini
hivyo kutokana na maombi hayo wataangalia ni wapi serikali imekwama ili
wao waweze kuongezea.
Kwa upande wao wanafunzi wamesema wameelewa namna
ggm inavyosaidia jamii na kuwa na mchango
mkubwa kwa serikali na wamefarijika na mafunzo waliyopata, huku baadhi ya
wanafunzi wasichana wakitamba kukabiliana na masomo ya sayansi
hii ni kufuatia hamasa waliyopewa.
No comments:
Post a Comment