Mamlaka ya Mapato
Tanzania TRA imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5319 yenye thamani ya Zaidi
ya Shilingi Million 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi baada ya
kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kuwa ni Salama kwa matumizi.
Sukari hiyo ilikamatwa
mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi ndani ya meli ya MV Hassanat
ikiingizwa kinyume cha Sheria ikitokea nchini Brazil kupitia Zanzibar.
Sukari hiyo ilipaswa
kulipiwa Kodi zaidi ya shilingi Million 246.
No comments:
Post a Comment