Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira na watu wenye ulemavu Dkt. Hamis
Mwinyimvua(Kushoto) akizungumza wakati wa akifungua mkutano wa wadau wa
biashara nchini uliolenga kujadili namna ya kuboresha mazingira ya biashara
katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania
Godfrey Simbeye na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Biashara(TNBC) Raymond Mbilinyi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Sekta Binafsi Tanzania Godfrey Simbeye(Katikati) akichangia hoja katika mkutano
wa wadau wa biashara nchini uliolenga kujadili namna ya kuboresha mazingira ya
biashara kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira
na watu wenye ulemavu Dkt. Hamis Mwinyimvua na kulia ni Katibu Mtendaji wa
Baraza la Taifa la Biashara(TNBC) Raymond Mbilinyi.
Wadau wa biashara kutoka sekta za umma na binafsi
wakifatilia mkutano uliofanyika leo uliolenga kujadili namna ya kuboresha
mazingira ya biashara nchini.
Serikali imedhamiria kuboresha mazingira ya biashara nchini ili
kuongeza uwekezaji na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa Kati.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira na watu wenye ulemavu Dkt. Hamis
Mwinyimvua wakati akifungua mkutano wa wadau wa biashara nchini uliolenga
kujadili namna ya kuboresha mazingira ya biashara.
Dkt. Hamis Mwinyimvua amesema Serikali imeazimia kuboresha
mazingira ya biashara nchini kwa kuandaa sera ambazo zitawasaidia
wafanyabishara kuwekeza katika sekta mbalimbali.
“Tutahakikisha tunaboresha mazingira ya biashara kwani hakuna
uwekezaji utakaowezekana kama mazingira ya ufanyaji wa biashara yatakuwa
hayaridhishi.” Alisisitiza Dkt Mwinyimvua.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Biashara(TNBC) Raymond Mbilinyi amesema kuwa kuna haja ya Taasisi zote za umma
na binafsi kufanya kazi kwa pamoja ili kuboresha mazingira ya biashara.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi
Tanzania Godfrey Simbeye amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano imeanza kufanya
maboresho katika mazingira ya uwekezaji.
Akifafanua kuhusu maboresho hayo Simbeye alisema kwasasa ujasili
wa makampuni unafanyika kwa kutumia mfumo wa kieletroniki ambapo muombaji anaweza
kusajili kampuni pasipo kufika katika Ofisi za BRELA katika kipindi cha muda
mfupi.
Mkutano huu uliondaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ikishirikiana na
Baraza la Taifa la Biashara, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania wakishirikiana
na taasisi za umma na binafsi umedhamiria kuwezesha wafanyabiashara na
wawekezaji kuwa mazingira mazuri ya kufanya biashara.
No comments:
Post a Comment