Baraza la
madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe mkoani Geita limemwagiza
mkurugenzi wa halmshauri hiyo James Ihunyo kukopa kiasi cha fedha cha
sh,milioni 500 kwenye taasisi za kifedha kwa
ajili ya kulipa fidia kwa maeneo ambayo hayajapimwa hususani maeneo ya Uyovu
na Namonge ambayo yanakua kwa kasi kubwa katika wilaya hiyo.
Diwani wa kata ya Bulangwa Yusufu Mohamed,ametaka
kujua kuwa yeye ni mjumbe wa kamati ya
ardhi lakini jambo ambalo limeendelea kuzua mjadala ,ni kwamba kamati hiyo haijawai kukaa na kujadili juu ya
changamoto ambazo wananchi wamekuwa wakikutana nazo katika swala la upimaji wa ardhi.
Akijibu
swali hilo mkurugenzi wa
halmashauri hiyo James Ihunyo,amesema
kuwa kamati hiyo kisheria inatakiwa kuwa
na afisa ardhi mteule na kwa sasa wilaya
ya Bukombe haina afisa huyo hali ambayo imekuwa
ikisababisha kutokukaa kwa kamati
hiyo.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Safari Mayala,amesema
kuwa hoja ya kukopa fedha kwa ajili ya kufidia ardhi ni
hoja ya muda mrefu ambayo imedumu kwa muda wa miaka minne hali hiyo ndio
iliyosababisha kumwagiza mkurugenzi kukopa ili waweze kufidia ardhi.
Aidha,mkurugenzi wa halmashauri hiyo ameongeza kuwa
suala la kukope fedha kwa ajili ya
kulipa fidia kwa wananchi wanaendelea kushughulikia na muda wowote wataanza kutoa fidia kwa wananchi
ili waweze kuachia maeneo ambayo kuna uwezekano wa kuwekwa kwa miradi mikubwa.
No comments:
Post a Comment