Wananchi mkoani Geita wamelalamikia kuwepo kwa tabia ya
kuchukuliwa watu wa mikoa ya nje katika
zoezi la usajili wa wafanyakazi wa umwagiliaji dawa za viuatilifu vya mbua.
Kutokana na kuwepo kwa malalamiko hayo Storm habari ilifanikiwa
kuzungumza na wenyeviti wa mitaa ambao ndio walikuwa wanafanya zoezi la kuwaandikisha
wananchi hao,wamesema kuwa kutokana na kuwepo na ubatili katika zoezi hilo ni
vyema likasitishwa ili usahili huo ufanyike kwenye nganzi
ya mitaa.
Kutokana na kuwepo kwa malalamiko hayo Storm habari ilibidi imtafute
,afisa afya wa halamashauri ya mji,Mabela Mabela,lakini aligoma kuzungumza kwa
madai kuwa anahitaji kupatiwa kibali na mkurugenzi.
Kutokana na majibu hayo Storm habari ilifika katika ofisi za
mkurugenzi lakini haikubahatika kumkuta baada ya kuambiwa kuwa amekwenda kwenye
kikao cha mkuu wa mkoa,na ilipo jaribu kuzungumza nae kwa njia ya simu alitoa
kibali lakini afisa afya akaendelea kugoma na mwisho wa siku aliondoka.
No comments:
Post a Comment