Kaimu Mkurugenzi
Idara ya Utamaduni Bi. Lily Beleko
kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akisisitiza jambo
wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu
maadhimisho ya siku ya Uanuwai wa Utamaduni yanayotarajia kufanyika Mei 21 mwaka huu ,kulia ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bw.Benjamini Sawe.
Kaimu Mkurugenzi
Idara ya Utamaduni Bi. Lily Beleko
kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akisikiliza swali
kutoka kwa mwandishi wa habari (hayupo
pichani) wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya Uanuwai wa
Utamaduni yanayotarajia kufanyika Mei 21
mwaka huu.
Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Uanuwai
wa Utamaduni Duniani Serikali imeitaka jamii kuhifadhi kulinda na
kuheshimu utamaduni wa nchi kwa vile ndio kitambulisho cha Taifa letu ili
kuweza kutambulika ndani na nje ya nchi.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi
wa Idara ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,utamadunu,Sanaa na Michezo Bi.Lily
Beleko wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu cha maadhimisho ya siku
ya Uanuwai wa Utamaduni Duniani ambapo kauli mbiu ya madhimisho ya
mwaka huu ni” Utamaduni wa Uadilifu na Nidhamu ya Kazi Huleta Maendeleo”, “Sasa
Kazi Tu”
.
Kaimu Mkurugenzi wa Utamaduni Bi.Lily Beleko amesema kuwa ni
wajibu kwa kila mtanzania kuheshimu Utamaduni wetu na
kushiriki kikamilifu katika kuutambua, kuujenga, kuuendeleza na
kuurithisha kwa vizazi vingine.
“Siku hii ni maalumu kwa kila mtanzaniana na kila mmoja hana
budi kukubaliana na harakati hizi za kulinda, kuhifadhi na kuendeleza Utamaduni
wetu kwa ajili ya vizazi vijavyo”Alisema Bi Lily.
Bi.Lily Beleko ameongeza kuwa nchi haiwezi kutambulika
na kuheshimika kama Taifa huru bila kuwa na Utamaduni wake hivyo
kuwepo kwa maadhimisho haya kunaipatia jamii fursa ya kuendelea kukumbushana
,kuhamasishana na kuhimizana katika kuuenzi utamaduni wa nchi.
Siku ya Uanuwai wa Utamaduni Duniani huadhimishwa
kila ifikapo tarehe 21 Mei, ambapo siku hiyo imeteuliwa na Baraza
kuu la Umoja wa Mataifa kuona umuhimu wa kuhifadhi na kuendeleza Utamaduni na
hivyo kupitisha Azimio Na 57/249 mnamo mwaka 2002.
No comments:
Post a Comment