Wafanyabiashara wa Soko Kuu
jijini Mwanza wameandamana kwenda
kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana ni baada
ya kikao chao na Mkurugenzi wa jiji kutokufikia muafaka.
Akizungumza na Storm habari Mwenyekiti wa Soko hilo Bw.Khamadi Nchola amesema kuwa kikao cha kutazama tenda upya kimeshindikana kufikia muafaka baada ya ofisi ya Mkurugenzi kubaki na msimamo wa
awali wa kupandisha kodi.
Awali wafayabiashara wenye meza na migahawa walilipa sh. elfu
10,000/= na sasa ni sh.elfu 50,000/= huku wa vyumba vya maduka na vioski sh.elfu
20,000/= sasa ni sh. laki 100,000/=kitendo amabacho wamekiita kuwa ni unyanyasaji
na kwamba wamelipeleka mbele ili lishughulikiwe
zaidi kabla ya hatua nyingine.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Bw.Adam Mgoyi
aliitisha kikao na kuketi na wafanya bishara
hao baada ya kutishia kugoma kutokana na mabadiliko ya malipo ya tozo za
pango na kuongezeka karibu mara nne sasa.
No comments:
Post a Comment