Wadau
mbalimbali mkoani Geita wametakiwa kuwasaidia watoto
yatima na wale
waishio katika mazingira magumu na sio kuiachia serikali pekee.
Hayo yamesemwa na
diwani wa kata
ya Buhalahala Musa Kabese wakati
alipokuwa akikabidhi sare za shule kwa wanafunzi waishio katika mazingira magumu katika shule
za msingi Mwatulole,, Nguzo mbili,, na Buhalahala ikiwa ni moja ya ahadi
zake alizoahidi kipindi cha kampeni.
Akitoa shukrani kwa niaba ya walimu,, mwl mkuu wa shule ya msingi Mwatulole
Catherini Mgusi amesema kuwa msaada huo utawasaidia watoto kujumuika na wenzao vizuri kwani hapo
awali walikuwa wakivaa sare zilizochakaa na kuonyesha baadhi ya sehemu za miili yao kitendo
kilichowafanya watoto hao kujisikia aibu.
kwa upande
wake mwenyeki wa shule hizo Lucas Kidengana amewaomba wafadhili kuisaidia shule hiyo ili
waweze kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo .
Aidha kwa upande wa wanafunzi wa shule hizo wametoa shukrani
zao baada ya kupokea msaada huo ambapo wamemuomba diwani Kabese kusaidia
kutatua na matatizo mengine yanayokabili shule hizo.
No comments:
Post a Comment