Mchezaji Thomas Ulimwengu |
Mchezo wa kirafiki wa kimataifa
kati ya wenyeji Kenya na Tanzania, Taifa Stars utapigwa kesho katika Uwanja wa
Moi Kasarani mjini Nairobi, Kenya kuanzia Saa 10:00 jioni.
Taifa Stars itaingia uwanjani bila mchezaji wake wa kulipwa Thomas Ulimwengu anaekipiga na TP Mazembe.
Kocha Mkuu wa Taifa
Stars , Charles Boniface Mkwasa atawakosa washambuliaji wake watatu
katika kikosi ambacho kitaivaa Harambee Stars.
Washambuliaji hao ni Mbwana Samatta kutoka Genk ya Ubelgiji,
Thomas Ulimwengu anayechezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC)
waliozuiwa na klabu zao na John Bocco ambaye aliumia mguu katika fainali ya
Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation
Cup, Azam ikifungwa na Yanga 3-1 Jumatano wiki hii.
“Madaktari wamempa Bocco saa 72
za mapumziko. Bila shaka kabla ya kucheza na Misri atakuwa amepona,” alisema
Mkwasa leo Mei 28, 2016 asubuhi na kuongeza kuwa Samatta ametuma taarifa kukosa
mchezo dhidi ya Kenya kwa kuwa ana ratiba ya kucheza mchezo muhimu Mei 30, mwaka
huu na matarajio ni kujiunga na timu Juni 1, 2016 kabla ya kuivaa Misri Juni 4,
mwaka huu.
Kwa upande wa Ulimwengu,
uongozi wa TP Mazembe nao waliomba kumtumia Ulimwengu katika mchezo wa
ushindani wa mpinzani wake AS Vita. TP Mazembe na AS Vita ni timu pinzani huko
DRC na TFF ikaridhia na Mkwasa sasa amejipanga kukiandaa kikosi bila nyota hao
mahiri.
“Katika mchezo huu sitakuwa na
professionals (wachezaji wa kulipwa),” alisema Mkwasa ambaye jioni ya leo
ameahidi kutoa kikosi cha nyota 11 watakaonza dhidi ya Kenya kesho.
Kwa sasa anaangalia namna ya kuipanga vema safu yake ya ulinzi baada ya kumkosa Kelvin Yondani anayetumikia adhabu ya kuonywa mara mbili kwa kadi ya njano hivyo kutojumuishwa kwenye mipango mchezo dhidi ya Misri. Mabeki anaotarajiwa kuanza nao ni Juma Abdul upande wa kulia na Mohammed Hussein upande wa kushoto.
Kwa sasa anaangalia namna ya kuipanga vema safu yake ya ulinzi baada ya kumkosa Kelvin Yondani anayetumikia adhabu ya kuonywa mara mbili kwa kadi ya njano hivyo kutojumuishwa kwenye mipango mchezo dhidi ya Misri. Mabeki anaotarajiwa kuanza nao ni Juma Abdul upande wa kulia na Mohammed Hussein upande wa kushoto.
Walinzi wakaoachukua nafasi ya
Yondani na Nadir Haroub Cannavaro ambaye hakuongozana na timu katika safari ya
Kenya ni Erasto Nyoni, Aggrey Morris na David Mwantika huku viungo wa kati wanaotarajiwa
kupangwa ni Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude na pembeni ni Farid Mussa na Shiza
Kichuya. Washambuliaji watakaotikisa Kenya katika mchezo wa kesho ni Elisu
Maguli na Ibrahim Ajib.
“Kipa anaweza kuanza Dida (Deo
Munishi) au Aishi Manula. Lakini hao niliokutajia ni proposed team (kikosi
tarajiwa), lakini hasa nani anaaza kesho nitakutajia jioni ya leo mara baada ya
mazoezi pale Moi Kasarani,” alisema Mkwasa aliyeonekana kujiamini na mipango
yake kama lilivyo jina lake la umaarufu la Master.
“Nimeiandaa timu kucheza mifumo
miwili ambayo ni 4-3-3 ambao ni mfumo wa kushambuliaji na pale tutakapokuwa
tuna-defense (tunazuia) basi mfumo utakuwa ni 4-5-1,” alisema Mkwasa.
Katika mchezo wa kesho Mkwasa anayesaidia na Hemed Morocco na Manyika Peter anayewanoa makipa atapata nafasi ya kubadili wachezaji hadi sita ambao ni utaratibu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa mechi za kirafiki za kimataifa kadhalika makubaliano katika mkutano wa kabla ya mchezo wa kesho.
Katika mchezo wa kesho Mkwasa anayesaidia na Hemed Morocco na Manyika Peter anayewanoa makipa atapata nafasi ya kubadili wachezaji hadi sita ambao ni utaratibu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa mechi za kirafiki za kimataifa kadhalika makubaliano katika mkutano wa kabla ya mchezo wa kesho.
Kamisaa wa mchezo atakuwa Amir Hassan kutoka Somalia ambako Meneja wa Uwanja wa Moi Kasarani, Lilian Nzile amesema kwamba mazingira uwanja ni mazuri na mipango yote ya mchezo huo imekaa vema ikiwa ni pamoja na usalama uliothibitishwa pia na Kanali wa Jeshi la Polisi, Muchemi Kiruhi OCS wa Kasarani.
Kipa Deo Munishi 'Dida' yuko
tayari kuanza kesho langoni dhidi ya Harambee Stars
|
Mchezaji aliyeitwa kwa mara
ya kwanza Taifa Stars, Hassan Kabunda (kulia) akiwa na mshambuliaji Elias
Maguri
|
Stars iliwasili Nairobi, Kenya jana asubuhi na kupokewa na wenyeji Shirikisho la Soka Kenya iliyowapeleka hoteli ya Nairobi Safari Club iliyoko mtaa wa Koinange, katikati ya jiji la Nairobi ambako mchana kabla ya kwenda mazoezi ilitembelewa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. John Haule aliyewahakikishia usalama timu hiyo licha ya kuwako kwa taarifa za kuvamiwa.
“Msaada wowote mnaotaka na
chochote mnachohitaji tunaomba mtutaarifu tujue namna ya kuwasaidia. Msiwe na
wasiwasi kabisa. Hata kama hamjaipenda hoteli, semeni,” alisema Dk. Haule
ambaye aliitakia timu mafanikio mazuri katika mchezo wa dhidi ya Harambee na
ule wa Mafarao wa Misri.
Viongozi wa msafara wa Taifa
Stars, Ahmed Mgoyi na Omar Walii walimweleza Balozi DK. Haule kuridhika na
kambi na kwamba hawakupata tatizo lolote hali ilivyo hadi sasa.
No comments:
Post a Comment