Mtu mmoja amefariki dunia na wengine kumi na mmoja kunusurika kifo baada ya kumaliza
kula chakula cha usiku.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jumatatu katika
kata ya Nyarugusu mkoani Geita ambapo inadaiwa kuwa watu hao baada ya chakula
cha usiku ambacho ni wali maharage walijikuta wakianza kuumwa na tumbo hali ambayo ilisababisha wote kwa pamoja
kuanza kuharisha.
Akizungumzia tukio hilo baba wa familia hiyo bw,
Gulamali Fungameza amesema kuwa baada ya hali hiyo kutokea waliamua kwenda
katika hospitali teule ya mkoa wa Geita ili kupatiwa matibabu lakini mmoja kati
ya watu hao aliyefahamika kwa jina la Rejiko Shija alifariki dunia kabla ya
kuanza kupatiwa matibabu.
Hata hivyo pia ,mmoja kati ya watu waliosalimika ,aliyejitambulisha
kwa jina la Joyce Johachim,amesema kuwa
tatizo hilo limetokana na mgonjwa ambae alikuja nyumbani hapo akitokea mjini Geita ambapo alifika akiwa na ugonjwa wa kuharisha na kutapika
hali ambayo ilisababisha familia nzima kujikuta wakiingia katika ugonjwa huo.
Aidha mganga mfawidhi wa hospitali teule ya rufaa
mkoani hapa dr. Adam Sijaona,amekiri kupokea wagonjwa hao na kwamba amedai hadi
kufikia hivi sasa chanzo cha tatizo hilo bado hakijafahamika.
cue…………..…………..sijaona
No comments:
Post a Comment