Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe mkoani Geita James Ihunyo amewaomba madiwani kuwaelimisha wananchi namna na jinsi
wanavyotakiwa kuhifadhi chakula ambacho kimepatikana kwa wingi katika msimu wa mavuno wa
mwaka 2015/2016.
Hayo ameyasema wakati wa kikao cha baraza la
madiwani wa kata zote katika
halmashauri hiyo kilichokuwa na
lengo la kupokea taarifa za kata na
namna na jinsi ambavyo kata hizo zimeweza kufanya kazi kwa muda wa miezi mitatu.
Ihunyo amesema
kuwa kutokana na wimbi la wafanyabishara
wanunuzi wa mazao kuvamia wilaya kumekuwepo na msongamano wa maroli
yanayofika vijijini huko kununua nafaka na mazao aina ya mikunde hali
ambayo imekuwa ikipelekea wananchi kujisahau na mwisho wa siku kuuza
mazao yote na wao kubaki hawana chakula ndani.
Aidha mbunge
wa jimbo la Bukombe ,mh Dotto Biteko amewaomba
madiwani kuendelea kumuunga mkono
rais John Magufuli katika mikakati yake ya
kufanya mabadiliko ya kweli kwa kuwa hadi sasa nidhamu kwa
watumishi imeanza kuonekana.
No comments:
Post a Comment