Miezi michache
baada ya Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) kujitoa kusaidia
Tanzania katika usambazaji wa umeme vijijini, Serikali ya Uingereza kupitia
taasisi yake ya Energy Africa Initiative, imetangaza utayari wa kutoa msaada
huo.
Waziri wa Uingereza wa Maendeleo ya Kimataifa, Justine Greening, ameeleza
utayari huo mwishoni mwa wiki, katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa, aliye nchini humo kumwakilisha Rais John Magufuli, katika mkutano wa
kimataifa wa kupambana na rushwa duniani. Katika mazungumzo hayo, Greening
alimhakikishia Waziri Mkuu Majaliwa, kwamba nchi yake iko tayari kuisaidia
Tanzania kwenye mpango wake wa kupeleka umeme vijijini.
“Tuko tayari kuwasaidia kutekeleza mpango huu
kupitia taasisi ya Energy Africa Initiative ambayo inapata ufadhili kupitia
Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID),” alisema.
Pia Waziri huyo wa
Uingereza, alipongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika
kupambana na rushwa na kwamba ndiyo maana Tanzania ilipewa mwaliko maalumu wa
kushiriki mkutano huo, kwa vile baadhi ya mataifa yanaziona juhudi zinazofanywa
na Serikali ya Rais Magufuli.
Aidha, alitumia fursa
hiyo kumpongeza Waziri Mkuu kwa nia ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imeionesha
katika kuwa na mpango wa kuendeleza viwanda.
Nguvu mpya Rea
Hatua hiyo ya Uingereza, imekuja wiki moja kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini Alhamisi wiki ijayo, ambayo mjadala wake utafanyika kwa siku mbili za Alhamisi na Ijumaa, unatarajiwa kuibua hoja ya kufutwa kwa msaada huo wa MCC wa Dola za Marekani milioni 472, uliokuwa utumike kusambaza umeme vijijini.

Mbali na mjadala huo
ambao unatarajiwa kung’ang’aniwa na Kambi ya Upinzani Bungeni, hatua hiyo ya
Uingereza itaongeza nguvu katika jitihada za Serikali zilizokwishaanza kwa
mafanikio za kuwapatia Watanzania umeme wa uhakika.
Taarifa za Wakala wa
Umeme Vijijini (Rea) zinaonesha kuwa, pamoja na MCC kujitoa Machi mwaka huu
katika usambazaji umeme, Serikali katika Bajeti ya 2015/ 2016 inayoisha Juni
mwaka huu, ilikuwa imeshatenga Sh bilioni 950 kwa ajili ya mradi wa Rea Awamu
ya Pili.
Mradi huo wenye lengo
la kufikisha umeme kwa vijiji 2,500 na kuunganishia nishati hiyo wateja 250,000
nchi nzima, unatarajiwa kukamilika Juni 30, mwaka huu na kupisha kuanza kwa Rea
Awamu ya Tatu, ambayo itaanza Julai mosi na kumalizika baada ya miaka
miwili.
Jitihada zote hizo,
lengo lake ni kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2015-2020,
ambayo inataka hadi ifikapo mwaka 2020, wananchi waliounganishwa na umeme
wafikie asilimia 60 na kiwango cha uzalishaji kifike megawati 4,915.
Mbali na malengo ya
Ilani hiyo, jitihada hizo pia zitachangia katika kutekeleza Dira ya Maendeleo
ya Taifa inayotaka Tanzania iwe nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025,
ambayo imeweka lengo la usambazaji umeme liwe asilimia 50 mwaka huo mwaka 2025
na asilimia 70 mwaka 2033.
Tayari Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ameshaelezea nia ya Serikali
kutaka sekta ya nishati itoe mchango mkubwa kufikia uchumi huo wa kati, kwa
kuwa rasilimali za kufikia lengo hilo kupitia nishati zipo na kinachotakiwa ni
dhamira na kasi ya kutekeleza.
Katika kusisitiza kasi
na dhamira hiyo ya Serikali, Waziri huyo amekuwa akielezea mafanikio
yaliyopatikana katika utekelezaji wa dira hiyo, iliyotaka ifikapo mwaka 2015
uunganishaji umeme uwe umefikia asilimia 30. Lakini, kutokana na utekelezaji
madhubuti wa dira hiyo, kiwango hicho kilivukwa lengo na kufikia asilimia 40
mwaka 2015.
JPM na Marekani
Mbali na msaada huo wa Uingereza katika kusambaza umeme vijijini, Serikali ya Marekani pia imeelezea kuvutiwa na utendaji wa Rais Magufuli katika kupambana na rushwa, hatua iliyoanza kuvutia wawekezaji wa nchi hiyo.

Naibu Waziri wa Mambo
ya Nje wa Marekani anayeshughulikia Masuala ya Kimataifa, Sarah Sewall, katika
mazungumzo yake na Waziri Mkuu Majaliwa nchini Uingereza katika mkutano huo wa
kimataifa, ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua katika mapambano dhidi ya
rushwa.
Alisisitiza kuwa
kampuni nyingi za Marekani, zimeonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania. “Ninaamini uwekezaji huu utasaidia
kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa watu. Tunampongeza Rais Dk Magufuli
kwa juhudi anazofanya na nipende kusisitiza kwamba ushirikiano baina ya
Tanzania na Marekani utaendelezwa katika maeneo yetu ya siku zote,” alisema.
Majaliwa
ashukuru
Akizungumza katika kikao chake na Waziri Sewall, Waziri Mkuu Majaliwa alimsisitiza asiache kusaidia kuwahimiza Wamarekani wengi waje kutalii Tanzania na wawekezaji zaidi waje kuwekeza nchini katika nyanja mbalimbali, ikiwemo uanzishaji wa viwanda, uongezaji thamani kwenye mazao yanayozalishwa nchini.

Alimhakikishia kuwa
Watanzania wamekuwa wakijifunza teknolojia mpya na za kisasa.
Kuhusu mafanikio katika mapambano na rushwa, Majaliwa alisema mkutano huo wa kimataifa, uliojadili jinsi ya kupambana na rushwa duniani, ni kiashiria tosha kwamba tatizo la rushwa ni kubwa na linataka juhudi za pamoja katika kukabiliana nalo.

Akizungumza na mawaziri
hao, Waziri Mkuu Majaliwa alisema kwamba viongozi wa Serikali wa Awamu ya Tano,
wameamua kwa dhati kupambana na kila ovu, linalotokana na janga la rushwa na
wameamua kuwajibika na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.
“Sasa hivi nchi yetu ina utamaduni mpya wa kufanya kazi na tumeamua
kufanya kazi kwelikweli na siyo tena kwa mazoea, tumeamua kuweka utamaduni mpya
wa kupiga vita rushwa, ili kuleta uwajibikaji na uwazi miongoni mwa watu wetu,” alisema.
Alipoulizwa nini
kimechangia kufanya Tanzania ing’are kimataifa katika vita hiyo, Waziri Mkuu
alijibu kwamba Tanzania imetumia mambo manne ambayo ni kuzuia rushwa isitolewe
ama kupokelewa, kampeni za kuelimisha jamii, kufanya mapitio ya sheria na
kuwepo kwa utashi wa kisiasa.
“Serikali inachukua hatua za kiutawala na
kisheria, kama vile kuanzisha Mahakama Maalumu ya Mafisadi ambayo inatarajiwa
kuanza kazi Julai mwaka huu,” alisema Waziri Mkuu.
No comments:
Post a Comment