Mratibu wa Miradi Plan International Geita Maxmillian Mtigwa akizungumzia dhamira ya shirika hilo kufadhiri semina hiyo.
Upungufu
wa majengo ya kusubiria uendeshwaji wa Kesi za watoto umetajwa kuwa miongoni
mwa changamoto zinazosababisha watoto wengi kupata hofu na kushindwa kutoa
ushirikiano na ushaidi katika Kesi zinazowahusu.
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Ezekiel Kyunga,
aliyewakilishwa na Mkuu wa wilaya ya Geita Bw Herman Kapufi wakati wa kufunga
Semina ya Wanasheria wakuu wa Serikali, waendesha mashitaka, Makarani wa Mahakama
na Askari polisi wa kitengo cha upelelezi na dawati la Jinsia kutoka wilaya
zote za Mkoa wa Geita.
Bw
Kapufi alisema watoto wengi hupata hofu pale wanapoona idadi kubwa ya Askari
mahakamani na kwamba lipo tatizom kwa wananchi kushindwa kutoa ushirikiano wa
ushahidi mahakamani.
"Upungufu wa majengo ni sababu ambayo inaonekana kuwafanya watoto kuwa waoga kwani wanapopelekwa polisi wanapowaona tu askali wanakuwa na uogo mimi nitaandika barua kwenye mamlaka usika ili kushughulikia tatizo hili"alisema Kapufi
Kwa
upande wake Wakili wa serikali Mkoani Geita Bw Emily Kiria amesema sheria ya
watoto ya mwaka 2009 haijaeleweka vizuri kwa wananchi na hivyo.
|
No comments:
Post a Comment