Baraza la Taifa
la Biashara (TNBC) limeandaa Mkutano wa 11 wa Baraza ambao utaongozwa na Rais
John Magufuli wiki hii.
Katibu Mtendaji wa
Baraza hilo, Raymond Mbilinyi, alisema jana kuwa mkutano huo unaonyesha dhamira
iliyonayo serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli ya kuweka mazingira
bora ya kufanya biashara na uwekezaji nchini.
“Mkutano huu wa Baraza
ni muhimu sana sekta za umma na binafsi kwani unatoa fursa kwa pande mbili hizi
kujadiliana namna bora ya kujenga mazingira ya biashara na kuvutia uwekezaji
zaidi kwa manufaa ya Watanzania,” Alisema Mbilinyi.
Alisema mkutano
utafanyika tayari kukiwa na mafanikio makubwa chini ya awamu ya Tano ambapo
viwanda zaidi 3,500 vikiwa vimeshaanzishwa katika kipindi kifupi tu cha uongozi
wa Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza.
“Huu utakuwa ni
mkutano wake wa pili kuuongoza kama Mwenyekiti wa Baraza tangu achaguliwe kuwa
Rais wa Awamu ya Tano. Mkutano wake wa kwanza umeleta mafanikio mengi katika
sekta za umma na binafsi,” Alisema na kuwa utafanyika Jumapili.
Mbilinyi alisema
serikali ya awamu ya tano imesimamia mabadiliko mbalimbali yaliyolenga
kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuhamasisha ujenzi wa uchumi wa kati
na viwanda.
No comments:
Post a Comment