Mtu mmoja wilayani chato mkoani geita amefariki
dunia baada ya kuliwa na mamba wakati alipo kuwa katika shughuli zake za uvuvi wa samaki katika ziwa victoria.
Tukio hilo limetokea
katika kijiji cha rubambangwe
wilayani chato ambapo mtu huyo
alikuwa katika shughuli zake za kila siku za uvuvi wa samaki ndipo alipo vamiwa na mamba kisha kumjeruhi vibaya katika sehemu zake za
mwili nakupelekea umauti.
Akizungumza mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Pasikali
Maliyatabu amesema kuwa kumekuwa na matukio ya mara kwa mara ya watu wanao
jishughulisha katika masula ya uvuvi wa samaki katika ziwa hilo
kukamatwa na kuliwa na mamba kwani tukio
hilo nila tatu kutokea katika kijiji
hicho ambapo siku za nyuma watu wawili warifariki dunia kwa kuliwa na mamba .
Aidha mwenyekiti
huyo amemtaja aliyefariki dunia kuwa ni Emmanuel John mwenye umri wa miaka 52
mkazi wa kijiji cha Rubambangwe wilayani chato.
Kwa upande wa baadhi ya wananchi wa kijiji
hicho Bw. Alex Nagabona na Bi.
Meresiana Bagaile wameiomba serikali kupitia halmashauri ya wilaya ya chato
kufanya utaratibu wa kuwaondoa wanyama wakali wanaoishi kandokando ya ziwa
hilo kwani wamekuwa tishio jambo ambalo
linawafanya kushindwa kufanya shughuli za uvuvi
huku wakihofia mamba pamoja viboko ambao wamekuwa wakijitokeza
mara kwa mara na kuleta madhara kwa wavuvi.
No comments:
Post a Comment