Thursday, 26 October 2017

WAKAZI WA WILAYA YA GEITA WALIOVAMIA HIFADHI ZA MISITU WAZIDI WAONDOLEWA

Eneo la hifadhi ya mistu likiwa limepandwa mahindi ambapo zoezi la kufyeka mahindi hayo likiendelea.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herma Kapufi akiongoza kikosi kazi cha kuwatoa wananchi ambao wamevamia kwenye Hifadhi ya mistu.

Tanuru la Mkaa likivurugwa kwenye mstu wa Samina

Eneo la hifadhi ambalo limekatwa miti ili kupisha shughuli za kilimo.

Kundi la Ng'ombe wakiwa wamekamatwa kwenye hifadhi ya misitu ya Samina.

Kibanda kikichomwa moto ambacho kilikutwa ndani ya hifadhi.


Nyumba ikiwa imebomolewa wakati wa zoezi la kuwaondoa wananchi 
walivyamia maeneo ya  hifadhi.





Serikali wilayani Geita imeendelea na zoezi la kuwaondoa baadhi ya wananchi waliovamia hifadhi za Misitu kwa kutoa na kuharibu mazao yaliyokuwa yamepandwa na kubomoa vibanda vilivyo ndani ya hifadhi. 
Zoezi la kuwaondoa wananchi hao kwenye maeneo ya hifadhi za misitu limeanza September 11 mwaka huu likiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo na wakala wa misitu, TFS.

Akizungumza wakati wa kuondoa mazao kwenye msitu wa Geita, Mwl Kapufi alisema lengo la serikali ni kuhakikisha misitu yote iliyo chini ya wakala wa Misitu nchini na ile ya Halmashauri inalindwa na kuendeleza uoto wa asili.

“Kuna wananchi ambao kwa kiburi wameingia kwenye maeneo ya hifadhi na kuendelea na shughuli za kilimo kikiwemo kilimo cha Nyanya ,Mahindi Mihogo na sisi tunachokifanya ni kuwaonesha kuwa unapokatazwa na serikali utakiwi kuwa mkahidi na siku ya wazee niliwaambia wananchi waache kuendelea na shughuli za kilimo kwenye maeneo ya hifadhi za mistu”Alisema Kapufi.

Kapufi,ameendelea kuelezea kuwa baada ya zoezi la kuwaondoa watu hao watafanya shughuli ya upandaji wa miti na kwamba wataakikisha wanawaimiza wananchi kila mmoja kupanda miti kwenye makazi yake isiyopungua kumi yakiwemo na maeneo ya mjini.

Meneja wa Wakala wa misitu wilayani Geita Bw Fred Nandika alisema wamefyeka zaidi ya ekari 300 za mazao ya mahindi, maharagwe na mihogo yaliyokuwa yamelimwa kwenye misitu ya hifadhi.

Na pia ameendelea kuelezea kuwa zoezi hilo ni endelevu na kwamba ni vyema kwa wananchi wakaachia maeneo hayo wazi na kuacha kusubiria kushurutishwa.
Baadhi ya wananchi wa maeneo ya Mgusu na Kayenze wamesema hatua ya serikali iko sawa lakini ni vema wangesubiri wananchi hao wakavuna kwanza mazao yao.

No comments:

Post a Comment