Serikali Mkoani Geita imesema kuwa haina tatizo na Mgodi wa Dhahabu
wa Geita (GGM) na kwamba haiwezi kuendelea kukubali jambo baya ambalo
linafanywa na mtu mmoja kuchafua sura ya mgodi mzima kwani shughuli
ambazo zimeendelea kufanywa zimeendelea kuleta manufaa kwa Taifa na mkoa kwa
ujumla.
Akizungumza baada ya ziara yake ya kutembelea na kuona namna ambavyo
mgodi huo umekuwa ukifanya shughuli za uzalishaji wa dhahabu,Mkuu wa mkoa wa
Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema mgodi na serikali ni kitu
kimoja kutokana na kwamba wamekuwa wakilipa fedha kwa Taifa pasipo kuwa na
udanganyifu wa aina yoyote.
“Hatuwezi tukakubali jambo lolote lile likafanywa na mtu moja likaonekana
uongozi wa mgodi na serikali kwamba hatuna mahusiano mazuri mimi napinga kwa
nguvu zote mgodi na serikali tuko kitu kimoja hawa ni wawekezaji wazuri
wanalipa fedha zinazotakiwa kwa wakati na kama kuna changamoto chache chache
zinaelezeka tukae pamoja tutatue”Alisema Luhumbi.
Kuhusu miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa na mgodi huo,Luhumbi
alisema kuna makosa mengi ambayo yalifanyika kwa miaka ya nyuma kutokana na
miradi ambayo ilikuwa ikipangwa wananchi walikuwa hawafahamu na kwamba kutokana
na timu ambayo imewekwa kwa sasa ya mgodi wanaamini miradi ambayo
imepangwa itatekelezwa kwa haraka na kwa
wakati zaidi.
“Makosa mengi yalifanyika katika miradi ya nyumba kosa moja ambalo
lilifanyika wewe huwezi kupanga mradi bila ya wananchi kuwa tayari wanafahamu
huo mradi na kuna maandalizi mazuri lakini kwa timu ambayo imetengenezwa kwa
wakati huu wakurugenzi wote wameshakaa na wamepitisha kwenye vikao halali
vya halmashauri kwa hiyo hili jambo lipo kisheria sana hapa tulipo kuna hatua
moja ambayo imebakia ya kuweka sahihi ili miradi ianze kutekelezwa”alisema
Luhumbi.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi amesikitishwa na
kitendo cha mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) kuandika barua kwa viongozi wa
makanisa ya Romani na AIC kukataza fedha za maendeleo kupelekwa kwenye miradi
suala ambalo sio kweli kutokana na sheria ya mwaka 2017 kubadilishwa ndio
chanzo ambacho kinapelekea fedha kujadiliwa na halmashauri husika.
Aidha Meneja mahusiano huo Tenga B Tenga
alisema lengo la mgodi ni kuhakikisha wananchi ambao wanauzunguka wananufaika
nao kwa nyanja mbali mbali zikiwemo za afya,uchumi pamoja na Elimu.
No comments:
Post a Comment