Watumishi wanne wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita wamesimamishwa kazi kwa tuhuma mbalimbali
Kikao
cha Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya nyang’hwale kilichofanyika Februari mosi na 02 kimewasimamisha kazi watumishi wanne wa idara
mbalimbali wilayani humo, mara baada ya kupatikana na tuhuma katika utendaji wao.
Akiwataja
watumishi hao mwenyekiti wa halmashauri
hiyo Aloyce Mussa Lumambi,amesema baadhi ya watumishi hao,ni pamoja na wakuu wa
idara mbili Bw. Donatus Pangani ambaye
alikuwa mkuu wa idara ya fedha na Dayness Mosha aliyekuwa mkuu wa Idara
elimu ya Sekondari.
Mkuu
wa wilaya ya Nyang’hwale Hamim Gwiyama amelipongeza Baraza hilo na ameongezea
kuwa bado kuna baadhi ya watumishi
wanafanya kazi bila kufata maadili ya kazi zao huku akitoa onyo kwa wale ambao hawatojali
maslahi ya wananchi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Carlos Gwamagobe amekiri
kusimamishwa kwa wafanyakazi hao.
No comments:
Post a Comment