Baadhi ya wakazi
wilayani Chato mkoani geita wametakiwa kuboresha vyoo vya asili kuwa vya kisasa kutokana na mvua za masika kuanza kunyesha ili
kuepuka vyoo hivyo kutitia na
kusababisha magojwa ya milipuko yanayo weza kujitokeza kutokana na uchafu wa
vyoo hivyo .
Rai hiyo
imetolewa na Mwenyekiti wa kijiji cha Mapinduzi Bw.Kitute Kalegea kijijini hapo ambapo amesema kuwa kuna idadi kubwa ya wakazi katika eneo hilo ambao wanatumia vyoo vya asili
ambavyo haviwezi kudumu kwa muda mrefu kutokana na miundo mbinu yake
kujengwa kwa kutumia udongo pamoja na miti.
Kalegea amewataka
wananchi ambao hawana vyoo katika
kjijini hicho wachimbe mara moja kwani
kume kuwepo na baadhi ya wakazi
katika eneo hilo ambao hawana vyoo katika familia zao na badala yake huduma
hiyo huipata katika vichaka vilivyo jiranai na nyumba zao jambo ambalo ni
hatari kwa afya zao pamoja na kijiji kizima kwa ujumla.
Aidha baadhi ya
wakazi katika kijiji hicho wamesema
kuwa kumekuwepo na idadi kubwa ya watu
ambao wanatumia vyoo vya asili jambo ambalo
ni hatari kutokana na vyoo hivyo kutitia wakati wa mvua za masika zinapo
anza kunyesha kitendo ambacho kinawafanya watumiaji wa huduma hiyo kukosa
sehemu rasmi ya kujisaidia na badala yake
wengine kutumia mifuko ya plasitiki
kwa kujikimu na mifuko hiyo mara nyingi hutupwa kando kando ya vyanzo vya maji pamoja na
barabara kitu ambacho kinaweza
kusababisha magonjwa ya milipuko kwa
baadhi ya wakazi katika kijiji hicho.
No comments:
Post a Comment