Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl. Herman Kapufi akizungumza na wananchi wa kijiji hicho
“ Kero ambayo imesababisha wananchi kugoma kuchangia madawati moja ni
kutokana na watendaji wambao walikuwa wanakuja wanakusanya michango wanaondoka
sasa tutaendelea paka lini unachanga kitu akifanyiki sisi tukaona ni bora
kugoma”Alisema Maningu
“Kiini ni kutokana na swala la ujenzi wa choo kutokukamilika wa shule ya
msingi Nyabalasana baada ya wananchi kuchanga na kuona kuwa kazi ijafanyika
inavyotakiwa ndio sababu ambayo imetupelekea kugoma”alisema Nzobe
Akisoma taarifa ya kijiji hicho Kaimu Afisa mtendaji wa kijiji
hicho Freda Bosha amebainisha namna ambavyo
mapungufu yalivyo kutokana na kukosekana kwa afisa mtndaji huku akimwomba mkuu
wa wilaya kupatikana kwa mtendaji kijiji hapo.
“Kukosekana kwa afisa mtendaji ni chanzo kikubwa cha mapato mengi kupotea
bila ya utaratibu Mh,Mkuu wa wilaya tunaomba kupatiwa mtendaji katika kijiji
ili aweze kusimamia shughuli za maendeleo kijijini hapa”alisema Bosha
Kufuatia hali hiyo iliyochangia hata uwajibikaji wa wananchi kuchangia
upande wa Madawati kusuasua, Mkuu wa Wilaya Mwl. Herman Kapufi pamoja na
kuwahimiza wakazi wa Nyabalasana kuendelea kujitolea
katika miradi ya maendeleo amewahakikishia kwa muda wa wiki mbili watampata
afisa mtendaji, huku akimwachia jukumu hilo Afisa utumishi.
“Lakini msiwe na tabia ya kuzira kwasababu ya
mtu fulani kama kuna tatizo mnakaa kwenye kikao mnajadili mnatafuta
mwafaka mwenyekiti inaonekana kuwa amezidiwa kutokana na kwamba akuna mtendaji
wa kijiji maana mtendandaji wa kijiji ndie mshauri bahati nzuri
afisa utumishi yupo hapa naamini hatalifanyia kazi kwani ndie mwenye uwezo wa
kuhamisha mtumishi”Alisema Kapufi
Katika hatua nyingine wakazi hao wakaliomba Shirika la Umeme Tanzania
{TANESCO} Mkoa wa Geita kupitia mradi wa Umeme Vijijini REA kuwafikishia
nishati hiyo.
Meneja wa Tanesco Mkoa wa Geita Joachim Ruweta akajibu maombi ya
wananchi amesema, serikali inampango wa kufikisha umeme katika vijiji
vyote vya Mkoa huo, ambavyo havikufikiwa kupitia mradi huo mkubwa wa REA awamu
ya pili.
“Wananchi wanatakiwa kuchangia kwa kuachia
maeneo yao wazi ili waweze kusababisha huduma kufika kwenye maeneo ya makazi
yao tunaendelea na jitihada za kusambaza umeme kwa awamu ya pili maeneo ambayo
bado umeme ujafika”Alisema Ruweta
No comments:
Post a Comment