Mwenyekiti
wa Bodi NHIF na Spika mstaafu wa Bunge mama Anna Makinda akisisitiza juu
ya huduma kuboreshwa katika mfuko wa Bima ya afya wa Taifa
Mkuu wa
Mkoa wa Geita,Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwa na mwenyekiti wa Bodi
ya NIHF wakisikiliza kwa makini taarifa ya Mkoa wa Geita juu ya mfuko wa bima
ya afya
Mkuu wa
Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akifungua mkutano wa
wadau wa Mfuko wa Bima wa Taifa Mkoani Humo
Kutokana na kuwepo kwa baadhi ya vituo vya afya kuwa na mazingira yasiyo
mazuri ya kimiundombinu na lugha chafu kwa baadhi ya hudumu wa
afya,ukosefu wa dawa na upungufu wa wataalam imeelezwa kuwa chanzo ambacho
kimekuwa kikisababisha juhudi za wananchi kutokujiunga na mfuko wa Bima
ya afya .
Akizungumza katika mkutano wa wadau wa afya Mkoani Geita mwenyekiti
wa Bodi NHIF na spika mstaafu wa Bunge Anna Makinda amesema wanafanya
maboresho ya kuhakikisha kila atakayejiunga awe na uwezo wa kupata huduma
kuanzia ngazi ya kijiji hadi Mkoani hivyo watumishi wachache wasiharibu fursa
ya wananchi kupata huduma nzuri.
“Inatakiwa mtu ambaye anakata NHIF aende akatibiwe kwenye ngazi ya zote
ndani ya Mkoa sio haishie kwenye zahanati ,zahanati zingine zimekuwa
zikikatisha tama unakuta mganga hayupo hata dawa hazipo jambo ambalo limekuwa
likiwakatisha tamaa wananchi ninachokisema wakurugenzi zungumzeni na wananchi
harafu tushirikiane katika mambo yafatayo lazima dawa ziwepo kituo cha afya
kiwe kituo cha afya kweli Mganga mkuu nadhani yupo hakikisha unafatilia haya
mambo kwa umakini zaidi”Alisema Mama Makinda
Hata hivyo kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa NHIF Angela Mziray
ameongezea kuwa Bado wananchi wanakabiliwa na magonjwa ambayo elimu hawana na
ukiangalia mfuko unaingia gharama ya asilimia 19 kutibu magonjwa
yasiyoambukiza.
“Kutokana na mtinda wa maisha
ambayo tumekuwa tukiishi kila siku unajikuta magonjwa ya siyoambukizwa yamekuwa
yanaongezeka kwa kiasi kikubwa sana sasa kutokana na hili mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya iliona ni vyema ukaboresha kwa kughalamia asilimia 19 za
matibabu kwa mgonjwa” Alifafanua Mziray.
Mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga
amewasisitiza watumishi wa sekta ya afya kuakikisha wanakuwa na maadili
ya kazi zao na kuachana na tabia ya ambazo zimekuwa zikiwakatisha tamaa
wagonjwa.
“Inatakiwa watumishi
katika vituo kujirekebisha na kuzingatia taratibu za kuadirifu kamavile
walivyoelekeza baada ya kuwa wameitimu mafunzo kuwa watafanya kazi kwa uadilifu
na pindi wanapofika kwenye vituowamekuwa wakichukua tabia ambazo sio nzuri kwa
wateja nah ii ni kutokana na majibu ambayo wamekuwa wakipatiwa wateja sio
mazuri”Alisisitiza Kyunga
Pamoja na serikali kusisitiza swala la watanzania kutumia
bima za afya bado tatizo ni kubwa kutokana na wengi wao kutokuwa na elimu
hivyo mamlaka husika zimetakiwa kutoa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa mfuko
wa Bima ya afya.
No comments:
Post a Comment