Chama cha mapinduzi (CCM) Wilayani Geita kimeadhimisha miaka arobaini (40) tangu kuanzishwa kwake
mnamo februari, mwaka 1977 kwa
kufanya shughuli ya ujenzi wa kituo cha Afya kwenye Kata ya shiloleli iliyopo
Halmashauri ya mji wa Geita.
Akizungumza na
wananchi kwenye shughuli hiyo ya
ujenzi wa kituo cha Afya mwenyekiti wa CCM
Wilayani hapa , Barnabas Mapande amemwambia
Muhandisi kusimamia kwa umakini ujenzi wa Boma isije
kutokea tatizo baada ya kuwa umemalizika Ujenzi.
Diwani wa kata ya Shiloleli,
Bonface
Kaswahili ameelezea pamoja na ujenzi huo kuendelea bado wanakabiliwa na changamoto
ya upungufu wa maji ya kujengea jengo hilo.
Kwa upande wa baadhi ya
wananchi ambao wamezungumza na Storm habari kuwa kukamilika ujenzi wa Kituo hicho cha Afya
kutarahisisha safari ya muda
mrefu kutembea kufuata huduma na kina
mama wajawazito kujifungulia njiani.
Aidha Katibu Mwenezi wa
Chama hicho, Jonathani Masele ameeleza kuwa Chama hicho kitaendelea kujitolea
kwa shughuli za wananchi ili kufata Ilani
ya uchaguzi ya mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment