Spika wa
Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Viongozi wa Kamati Tendaji ya
Skauti waliomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam mapema leo. Wa
pili kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia
Mhe Eng. Stella Manyanya (Mb) na anayefutia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji
ya Skauti Tanzania Balozi Nicholas Kuhanga.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia
Mhe Eng. Stella Manyanya (Mb) aliyeambatana na Viongozi wa Kamati Tendaji ya
Skauti Tanzania akimueleza jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai wakati
walipotembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Skauti
Tanzania Balozi Nicholas Kuhanga akimueleza jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai
wakati walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (aliyekaa kulia)
na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia Mhe Eng. Stella
Manyanya (Mb) katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Skauti
Tanzania mara baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Job Ndugai amewaahidi
Viongozi wa Chama cha Skauti Tanzania ushirikiano katika utekelezaji wa
shughuli mbalimbali za chama hicho ikiwemo maadhimisho ya Siku ya Skauti Afrika
na Maadhimisho ya miaka mia moja ya Skauti hapa nchini.
Mhe Spika aliyasema hayo wakati alipokutana na
kuzungumza na Viongozi wa Kamati ya Utendaji
ya Skauti Tanzania Ofisini kwake Jijini
Dar es Salaam ambao walimuomba awaunge mkono katika shughuli zao.
Spika Ndugai aliwaeleza Viongozi hao kwamba kwa
niaba ya Wabunge wote ameupokea ujumbe huo na atajitahidi sana katika
kuhufikisha kwa Waheshimiwa Wabunge.
“Ninawashukuru sana kwa ujumbe huu na niwaahidi
kwamba tupo pamoja si katika hili tu bali katika mambo yoyote ambayo mtakuwa
mkiyafanya na nawaahidi pia ushiriki wa Waheshimiwa Wabunge katika maadhimkisho
hayo,” alisema Mhe Spika.
Awali akimuelezea Mhe Spika kuhusiana na Shughuli
mbalimbali za Skauti hapa nchini Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia
Mhe Stella Manyanya ambaye aliambatana na Viongozi hao wa Skauti alisema pamoja
na majukumu mengine Chama hicho cha Skauti kina kazi kubwa ya kuandaa maadhimisho
ya Siku ya Skauti Dunia na Maadhimisho ya miaka mia moja ya Skauti hapa nchini.
Mhe Manyanya alisema kuwa maandalizi ya Maadhimisho ya siku Skauti Afrika ambayo
yanatarajiwa kufanyika tarehe 8 hadi 11 Machi mwaka huu mkoani Arusha
yanaendelea vizuri ingawa kuna changamoto kubwa ya kifedha katika maandalizi ya
maadhimisho ya miaka mia moja ya Skauti hapa nchini ambayo yanatarajiwa
kufanyika kuanzia Juni hadi Julai Mkoani Dodoma.
“Mhe Spika kumekuwa na jitihada mbalimbali za
kufanikisha maadhimisho haya lakini kumekuwa na changamoto katika kufikia
malengo na ndio maana tumefikana hapa ili kukuomba utuunge mkono” alisema Mhe
Manyanya.
Mhe Manyanya aliongeza kuwa Wizara imendelea
kutambaua kazi kubwa ambayo Chama cha Skauti inafanya katika kuendelea kuhimiza
nidhamu miongoni mwa Vijana na kuwajengea moyo wa kujitolea.
“Chama hiki Mhe Spika kimekuwa kikiendelea kufanya
kazi kubwa katika kuwajengea Vijana wetu moyo wa kujitolea na kwa sasa tunataka
kazi zao zifanyike kwa nguvu zaidi tofauti na hapo mwanzo”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Skauti
Tanzania Balozi Nicholas Kuhanga alisema anathamini sana mchango wa Mhe Spika
na kwamba anashukuru kwa kauli yake ya kuwaunga mkono.
Balozi Kuhanga aliongeza kuwa kwa sasa Uongozi wake
unajipanga katika kuhakikisha kuwa Skauti inazidi kukua hapa nchini.
“Mhe Spika nia ni kuona Vijana wa Shule za Msingi
hadi Chuo Kikuu wanaingia katika Skauti na hivyo tunataka twende mbele zaidi ya
hapa tulipo kwa sasa,” alisema Balozi Kuhanga.
No comments:
Post a Comment