Baadhi ya wananchi
mkoani geita wameahidi
kushirikiana na serikali kikamilifu kupiga vita uuzaji wa dawa za kulevya kwani zimeleta athari kubwa kwa vijana pamoja na watoto wadogo katika
taifa.
Hatua hiyo imekuja
baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka
katika jiji hilo kuanzisha kampeni maalumu ya kutokomeza uzaji
na usambazaji wa dawa hizo.
Hali hiyo imepelekea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
kumuapisha Kamishina Rogers Sianga
kwa lengo la kupambana vikali
dhidi ya watu ambao wanaji husisha
na uzaji wa dawa za kulevya nchini.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Bwana
Selemani Pinde mkaazi wa geita mjini yeye ni mmoja kati ya watu ambao
wamepoteza ndugu zake kutokana na athari
za madawa ya kulevya
Kwa upande wake Katibu wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya
ya Geita Bw. Ally Rajabu ameahidi
kushirikiana na Serikali kikamilifu kwa lengo la kutokomeza uuzaji
na usambazaji wa dawa hizo.
Aidha Diwani wa kata ya Buhalahala Bw. Mussa
Eliasi amewataka vijana ambao hawana kazi kujiunga katika vikundi
mbalimbali ambavyo vinaweza kusababishia kupata mikopo na kufanya biashara ndogondogo kuliko kukaa mitaani jambo ambalo linapelekea kujiunga katika makundi mabaya
kama ya utumiaji wa dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment