Askofu wa Good News for All Ministry Dkt. Charles Gadi kwa niaba ya dini na madhehebu mbalimbali hapa nchini wamempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua Kamishna wa Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Dkt. Gadi ametoa pongezi hizo leo, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na vyombo vya habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO).
“Tunamshukuru Mungu
kwa kumuinua Rais ambaye ameonyesha nia na kuwa mstari wa mbele kupigana
na biashara hiyo haramu, ni ukweli usiopingika kwamba tatizo la dawa ya
kulevya ni kubwa na lenye madhara makubwa sana kwa watanzania wengi
haswa vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa,” alifafanua Dkt. Gadi.
Aliendelea kwa kusema
kuwa, Vijana wengi wamepoteza maisha , kuharibika akili, kupata magonjwa ya
kuambukiza, kupoteza malengo ya kimaisha kwa sababu ya dawa hizo.
Vile vile dawa hizo zimeleta fedheha kwa Taifa kutokana na Vijana wengi wa
Kitanzania kuwepo katika magereza mbalimbali Duniani huku wengine
wakisubiri adhabu ya kunyongwa.
Aidha amempongeza Rais
Dkt. Magufuli kwa kuimarisha Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za
Kulevya kwa kumteua Kamishna ambaye atasimamia Mamlaka hiyo na
anaamini kwamba kwa neema ya Mungu ataweza kumsaidia kikamilifu Rais
Magufuli katika kutimiza azma yake ya kukomesha biashara hiyo.
Wakati huo huo, Dkt.
Gadi amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuianzisha vita hiyo dhidi
ya matumizi ya dawa kulevya katika mkoa wa Dar es Salaam. Vile vile
amewapongeza waandishi wa habari na vyombo mbalimbali vya habari kwa kutoa
habari zinazosaidia katika upambanaji wa biashara hiyo.
Dkt. Gadi amewataka
viongozi wa Dini kuungana bega kwa bega na Rais Magufuli kwa kuendelea kutoa
maadili kwa vijana ili kuepukana na uovu wa dawa za kulevya nchini.
No comments:
Post a Comment