Wakazi katika Kata ya
Buseresere wilayani Chato mkoani Geita wameiomba Serikali kuwaboreshea
miundombinu ikiwa ni pamoja na mitalo ya kusafirisha maji taka ili kuepuka
kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na mvua za masika kuanza kunyesha.
Hatua hiyo imekuja
baada ya mvua za masika kuanza kunyesha kwa kasi katika eneo hilo jambo ambalo
limesababisha maji kutuama katika makazi ya watu kutokana na ujenzi holela huku
watoto wadogo wakihofiwa kufa maji kutokana na maji hayo kutuama katika mshimo ya taka yaliyopo karibu na makazi ya watu.
Wakizungumza na Storm
habari mapema hii leo kijijini hapo baadhi ya wakazi katika eneo hilo wamesema
kuwa wanaiomba serikali kuwaboreshea miundo mbinu itakayo wezesha maji kuto tuama
katika makazi ya watu kwani hali hiyo inakwamisha shughuli za kiuchumi
kutofanyika hasa vyumba vya kulala wageni kukosa wateja kutokana na kujaa maji.
Kwa upande wake
Mzee Shaaban Abeid ambae ni mwenyeji wa eneo hilo na
aliwahi kuwa Afisa mtendaji wa kata ya Buseresere amesema kuwa madhara ambayo
yanaweza kujtokeza kutokana na maji kukosa njia ya kupitia ni pamoja na nyumba
zao kubomoka hasa kwa mvua zinazo nyesha nyakati za usiku.
Aidha Afisa mtendaji
wa kijiji cha Buseresere Bw. Issa Mohamed Husein amesema kuwa kumekuwa na idadi
kubwa ya nyumba ambazo zime jengwa kiholela katika eneo hilo na ameiomba
serikali kupitia halmashauri ya wilaya
ya chato kuboresha miundombinu ikiwa ni pamoja na kupanga kijiji hicho ili
kuondokana na adha kama hizo.
No comments:
Post a Comment