Zaidi ya nyavu haramu 495 zenye thamani ya milioni
85 laki mbili na elfu 78
zimekamatwa wilayani chato mkoani geita
katika msako mkali ulioongozwa na
maafisa uvuvi pamoja na mkuu wa wilayani hiyo kwa lengo la kutokomeza uvuvi
haramu ulioshamili katika ziwa victoria
Wilaya ya chato ni sehemu ambayo ina idadi
kubwa ya wavuvi wa samaki ambapo kuna jumla ya wavuvi 3336 na mitumbwi
1112 pamoja na mialo 36
kutokana na hilo kumekuwepo na baadhi ya wavuvi ambao hawafuatai sheria
na taratibu za uvuvi na badala yake kukiuka na kuanza kutumia uvuvi haramu
kitendo ambacho kinaweza kupelekea
kutokomeza samaki katika ziwa victoria.
Kutokana na hilo viongozi pamoja na baadhi ya
wavuvi wameweka mpango mkakati wa
kuhakikisha suala hilo wanalishughulikia kikamilifu ili kutokomeza uvuvi
haramu ulio kithiri katika eneo hilo.
Wakizungumza baadhi ya viongozi wa wavuvi wamepongeza juhudi za viongozi wa eneo hilo
kwa kukamata nyavu haramu katika eneo
hilo kwani bila kufanya hivyo wimbi la
wavuvi haramu linge kuwa linaongezeka
kila kukicha.
Kwa upande wao
maafisa uvuvi Bi.Damali Charles pamoja na Makisensio Masasi katika kata
ya Nyamirembe wilayani chato wamesema watapambana kikamilifu ili kuhakikisha
wanatokomeza suala la uvuvi haramu wilayani humo.
Aidha mkuu wa wilaya ya chato Bw. Shabani Ntarambe amesema kutokana na agizo hilo kupewa na makamu wa
raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Bi. Samia Hassan la kuhakikisha anamaliza uvuvi haramu katika eneo hilo,
suala hilo atalivalia njuga na kwa kiongozi yeyote katika wilaya hiyo atakae
shinndwa kutimiza majukumu yake kwa wakati kuhusiana na zoezi hilo la kupambana
na uvuvi haramu hatua kali za sheria zitachukuliwa dhidi yake.
No comments:
Post a Comment