Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Sheria mkoani Geita
Jamii ya wanasheria Mkoani Geita imetakiwa kutoa haki kwa misingi
na sheria ikiwa ni pamoja na kuzingatia swala la muda kwenye kesi ambazo
wanazisimamia.
Kauli hiyo imesemwa na wakili wa serikali Mkoani humo Emily Kiria
wakati wa maadhimisho ya wiki ya sheria, ambapo ameeleza kuwa jamii ya
wanasheria wote wawe wa serikali na wakujitegemea wanajukumu la
kuhakikisha wanatoa haki kwa uharisia na ukweli kwa swala usika.
“Jamii ya wanasheria na hili ni
jukumu la wanasheria wote wawe wa serikali au wa kujitegemea wanalo jukumu la
kuhakikisha wanatoa haki kwa uharisia na kwa ukweli wa swala usika na siyo
kuhakikisha tu kwamba wanawatetea au kuwasaidia watu kwasababu tu wamefika
kuomba msaada”alisema Kiria
Kwa upande wake wakili kutoka chama cha mawakili Tanzania(Tanganyika law
society),Bernad Otieno,alifafanua kuwa mahakama inawajibu wa kusikiliza
malalamiko yanayoletwa na wananchi na kuyatolea mahamuzi wajibu huo ni wa
kikatiba kwani inatokana na jamhuri ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa
marekebisho katiba ibara ya 107 (A) ibara ndogo ya kwanza na ya pili.
Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho
hayo ,Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,ameendelea kusisitiza swala la muda
wa kusikiliza kesi ,pamoja na kuwataka watumishi wa mahakama kuwa
wahadilifu na waaminifu kwenye shughuli zao.
“Naomba kutoa wito kwa watumishi
kuendesha kesi kwa muda usika ikiwa ni pamoja na kuwa waaminifu katika shughuli
zenu za kila siku za kutoa haki kwa wananchi”alisisitiza Kyunga
Siku ya Sheria nchini ilioanzishwa mwaka 1996 ikiwa ni siku muhimu ya
kuombea Majaji na Mahakimu ili kuweza kusikiliza kesi ambapo kitaifa
imefanyikia jijini Dar es salaam na Mgeni Rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli,kauli mbiu ikiwa ni Utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.
No comments:
Post a Comment