Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu(NBS) Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) kuhusu kuongezeka kwa mfumuko wa bei leo jijini Dar es Salaam. Mfumuko
wa bei umeongezeka kutoka asilimia 5.0 kwa mwezi Desemba mwaka jana hadi
kufikia asilimia 5.8 mwezi januari 2017.
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu(NBS) Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) kuhusu kuongezeka kwa mfumuko wa bei leo jijini Dar es Salaam. Mfumuko
wa bei umeongezeka kutoka asilimia 5.0 kwa mwezi Desemba mwaka jana hadi
kufikia asilimia 5.8 mwezi januari 2017.Kulia ni Kaimu Meneja wa Idara ya
Takwimu za Ajira na Bei Bibi. Ruth Minja.
Mkurugenzi wa Sensa na
Takwimu za Kijamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) Ephraim Kwesigabo
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuongezeka kwa mfumuko wa bei leo
jijini Dar es Salaam. Mfumuko wa bei umeongezeka kutoka asilimia 5.0 kwa mwezi
Desemba mwaka jana hadi kufikia asilimia 5.8 mwezi januari 2017.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano kuhusu Takwimu za
mfumuko wa bei kwa mwezi Januari zilizotolewa na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu
za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo (hayupo
pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nchini
Tanzania umeongezeka kwa kiasi kidogo ukilinganisha na nchi za Afrika
Mashariki.
Takwimu hizo zimetajwa leo Jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBC), Ephraim Kwesigabo alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mfumuko wa bei za bidhaa na huduma
kwa mwezi Januari mwaka 2017.
Kwesigabo amesema kuwa nchi zote za Afrika Mashariki
hali ya mfumuko wa bei huwa unafanana na kwa kawaida Tanzania inajilinganisha
na nchi za awali za Kenya na Uganda kwa sababu nchi zingine zina tofauti kidogo
katika utoaji wa takwimu zao.
“Takwimu zilizoishia mwezi Disemba mwaka 2016, zinaonyesha
kuwa nchi ya Uganda mfumuko wa bei umeongezeka kutoka asilimia 5.7 hadi
asilimia 5.9 na nchini Kenya umeongezeka kutoka 6.35 asilimia hadi asilimia 6.99 hivyo kwa ujumla mfumuko
wa bei Tanzania ni mdogo,”alisema Kwesigabo.
Ameongeza kuwa, farihisi za bei zimeongezeka kutoka
100.71 mwezi Januari, 2016 hadi 105.92 mwezi Januari, 2017 wakati mfumuko wa bei
za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Januari,2017 zimeongezeka hadi
asilimia 7.6 kutoka asilimia 7.0 ilivyokuwa mwezi Disemba, 2016.
Kwa takwimu za mwezi kwenye upande wa mfumuko wa bei
za bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za
vyakula, Mkurugenzi amefafanua kuwa bei za vyakula nyumbani na migahawani zimeongezeka
kutoka asilimia 7.4 mwezi Disemba 2016 hadi kufikia asilimia 8.2 kwa mwezi Januari
2017.
Aidha, badiliko la farihisi za bei kwa bidhaa zisizo
za vyakula limepungua hadi asilimia 3.6 mwezi Januari,2017 kutoka asilimia 3.8
mwezi Disemba 2016.
Mfumuko wa bei nchini kwa kipimo cha mwaka
umeongezeka hadi asilimia 5.2 wakati mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi
Januari, 2017 umeongezeka kwa asilimia 0.8.
No comments:
Post a Comment