Kutokana na kauli ya
Raisi wa Jamhuli ya muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli yakupiga marufu unywaji wa pombe nyakati za asubuhi,
hali hiyo imekuwa tofauti katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro ambapo
kumekuwa na baadhi
ya watu ambao wanajihusisha na vitendo hivyo badala ya kutumia muda huo kuwa
kazini.
Akizungumza mwenyekiti
wa mamlaka ya mji mdogo wa Katoro Wilayani na Mkoani Geita Bw. Japheti Madoshi amesema
kua amepiga marufuku uuzaji wa pombe za kienyeji kiholela pamoja na kuwaomba wananchi
kutojihusisha na unywaji wa pombe nyakati za asubuhi na badala yake
wajishughulishe katika shughuli mbalimbali kwani bila kufanya hivyo hatua kali za
kisheria zitachukuliwa kwa mtu atakae
kiuka agizo hili.
Aidha baadhi ya wakazi
katika eneo hilo wamepongeza juhudi za serikali ya mamlaka ya mji mdogo wa Katoro
kwa kupiga marufu unywaji wa pombe nyakati za asubuhi hali ambayo itapelekea
baadhi ya watu wenye tabia hiyo kuacha
mara moja na kujishughulisha katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo .
No comments:
Post a Comment