Wafanya biashara wa samaki wilayani Chato mkoani Geita
wameiomba serikali kupunguza bei ya kuchukulia lesseni ya kuendesha
shughuli hiyo ya uzaji wa samaki kutokana na bei hiyo kuwa juu zaidi .
wakizungumza jana baadhi ya wafanya biashara katika
soko la chato mjini wamesema kuwa kumekuwa na changamoto nyingi katika
uendeshaji wa biashara hiyo wilayani
humo kutokana na ushuru ulio kithiri jambo ambalo limepelekea baadhi ya
wafanya biashara kukimbia soko hilo.
wafanya biashara hao wameiomba serikali kupitia
halmashauli ya wilaya ya chato kupunguza kodi
zisizo kuwa za lazima ili kuweza kufanya biashara hiyo kwa kufuata
misingi na taratibu zitakazo wafanya kunufaika na biashara hiyo.
kwaupande wake mwenyekiti wa soko hilo bw. Daudi Francisco
ameiomba Serikali kuliangalia na kulifanyia kazi suala hilo kwani
hali hiyo inasababisha kupunguza mapato katika eneo hilo kutona na
baadhi ya wafana biashara kuacha kufanya biashara hiyo kwa sababu ya kodi zilizo kithiri .
No comments:
Post a Comment