Vyuo Vikuu hapa Nchini vimeagizwa kuacha mara moja kutoza ada kwa fedha za kigeni kwa wanafunzi ambao ni watanzania.
“Sarafu inayotakiwa
kutumika Tanzania ni shilingi ya Kitanzania kwa mujibu wa kifungu cha 25 na 26
cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ya mwaka 2006. Aidha, kwa Tanzania
malipo ya kitu au huduma yoyote inapaswa kulipwa kwa shilingi ya Kitanzania
kama ilivyoainishwa kwenye kifungu cha 28 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania,
2006,” alifafanua Mhandisi Manyanya.
Aliendelea kwa kusema
kuwa japo Wizara haijapokea malalamiko yoyote ya kutozwa fedha za kigeni kwa
wanafunzi wa Elimu ya Juu tangu itoe agizo kama hilo kwa wamiliki wa vyuo
Septemba 07, 2016.
Hivyo basi kwa mara
nyingine Mhandisi Manyanya ameviagiza vyuo ambavyo bado vinatoza wanafunzi
Watanzania fedha za kigeni kuacha mara moja kwani vyuo hivyo vimeelekezwa
kutoza wananchi wa Kitanzania kwa pesa ya Kitanzania.
Aidha Mhandisi
Manyanya amewataka watanzania kutoa taarifa Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia ikiwa kuna Chuo chochote kinachotoza ada kwa Watanzania kwa fedha
za Kigeni ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.
No comments:
Post a Comment