Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante
Ole Gabriel akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo Pichani) leo Februari
07, 2017 jijini Dar es Salaa kuhusu mkakati wa Wizara kuanza kuzungumza na
wadau kuhusu mambo mbalimbali katika sekta zinazosimamiwa na Wizara yake.
Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo imebuni na kutanganza Programu ya kushirikisha wadau inayoitwa
wadau tuzungumze itakayosaidia wizara kupata vionjo, maoni, mawazo na fikra za
wadau katika kuhakikisha kwamba Wizara inafanya kama wadau wake wanavyotegemea.
Hayo yamesemwa na
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel alipokua akizungumza na waandishi wa habari kutangaza programu hiyo
yenye kauli mbiu ya kuitoa wizara ofisini kuipeleka kwa wadau leo Jijini Dar es
Salaam.
Prof. Gabriel amesema
kuwa Wizara imekua na kauli mbiu ya kuitoa Wizara Dar es Salaam kuipeleka
mikoani na sasa inaendelea na mkakati wa kuitoa wizara ofisini na kuipeleka kwa
wadau kwani Shabaa kubwa ya wizara ni kuhakikisha kwamba yale yanayofanywa na
wizara jamii iyafahamu katika kutekeleza nia na hari ya hapa kazi tuu ya
serikali ya awamu ya tano.
“Mpango wa programu ya
wadau tuzungumze utafanyika kisekta ambapo utakua ni mkutano utakaoshirikisha
mmoja wa viongozi wa wizara kukutanana na wadau na utakua na utaratibu
madhubuti kwa kila mwezi siku ya jumanne saa nne asubuhi ambapo viongozi hao
watakutana na vyombo vya habari wakiwa na wadau kujadili mambo ya kisekta”
amesema Prof. Gabriel
Mpango huu utahusisha
Jumanne ya kwanza ya mwezi sekta ya habari na wadau wote wa habari, jumanne ya
pili ya mwezi ni kwa ajili ya sekta ya Utamaduni na wadau wote wa utamaduni,
jumanne ya tatu ya mwezi ni kwa ajili ya sekta ya sanaa na wadau wote wa sanaa
na mwisho jumanne ya nne ya mwezi ni kwa ajili ya sekta ya maendeleo ya michezo
na wadau wake.
Pamoja na mambo
mengine program hii itatoa fursa kubwa sana kwa wadau kuleta mawazo yao ili
wizara iweze kuwaingiza kwenye mnyororo wa thamani wa shughuli zake kwani
wizara inatamani ifanye kwa mlengo ambao wadau weke wanatamani ifanyike.
Progamu
hii itazinduliwa rasmi tarehe 14 Mwezi Februari mwaka 2017 hapa Jijini Dar
es Salaam ambapo itahushisha sekta ya Utamaduni na hapo baadaye mikutano hii
inaweza kufikiriwa na kufanywa kwa kanda. Mpango huu utahusisha pia Taasisi
zilizo chini ya wizara.
No comments:
Post a Comment