Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja
Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga amefanya ziara ya kutembelea vijiji
na mitaa katika wilaya ya Geita lengo likiwa ni kuzungumza na kujua wananchi
ambao wanapatiwa fedha kutoka kwenye mfuko wa kunusuru kaya masikini (TASAF )wanavyofaidika
na fedha hizo na namna ambavyo wamezifanyia kazi.
Kyunga
ametembelea kwenye kata za Busanda, Nyakamwaga, Nyanguko, Mtakuja na Bumwangoko
na kusitiza wananchi ambao wanapatiwa
fedha hizo kutoka kwenye mfuko huo kutumia kwa maendeleo ambayo
yatawasaidia hata baada ya kuwa muda umemalizika wa kupatiwa ruzuku.
Aliongeza
kuwa mpango huo sio wa kudumu ni wa miaka mitatu na kwamba hadi sasa wamelipwa
awamu kumi hivyo wamebakiza awamu nane za kulipwa hivyo amewataka
kuhakikisha muda uliobaki wanatumia fedha kwa manufaa
Hata
hivyo baadhi ya wanufaika wa mradi huo wamesema kuwa tangu kuanzishwa
wamefaidika na vitu vingi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba pamoja na
kusomesha watoto hivyo kutokana na hatua hiyo wameishukuru serikali kwa maana
imeweza kuwasaidia wale ambao walikuwa awana uwezo.
Pia
katika ziara yake ya siku mbili mkuu wa
mkoa wa geita,amekutana na changamoto ya wanufaika wa mradi huo kutokujua
kikomo cha kupokea fedha na wengine kushindwa kutimiza makusudio ya fedha
hizo kama ambavyo zimepangwa kufanya shughuli za kimaendeleo na kunusuru kaya
ambazo hazina uwezo wa kifedha na kipato na wale ambao walishindwa kuwasomesha
watoto
No comments:
Post a Comment