Mkuu wa
wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akizindua zoezi la upigaji wa picha kwa wazee
pamoja na vitambulisho.
Baadhi ya
wazee wakiwa kwenye uzinduzi wa kupatiwa vitambulisho vya matibabu ambavyo
vitatoa masaada wa kutibiwa bure kwenye Hospitali,Zahanati na vituo vya afya
vya hapa nchini.
Wazee katika kijiji na kata ya nyamogota wilayani Geita,wamesema kuwa
bado wanakabiliwa na ukosekanaji
wa huduma bora ya afya pamoja na kuwepo kwa dirisha
la wazee ambalo linatoa nafasi ya kuwasikiliza wilayani humo.Wakizungumza wakati wa zoezi la upigaji picha wazee
kwaajili ya vitambulisho vya matibabu na uhamasishaji wa mfuko wa afya ya jamii Mzee James Magazi na Ramadhani Shaban,wamesema kuwa bado changamoto ni kubwa kwa wazee kutokupewa kipa umbele kwenye huduma ya afya.
“Kiukweli pamoja na kwamba serikali imeweka utaratibu wa madirisha ya wazee ambayo yatatoa msaada wa kuwasikiliza wazee lakini bado
tunachangamoto nyingi sana kwani huduma ya afya bado nitatizo kutokana na kukosekana kwa madawa kwenye zahanati na vituo vya afya tunavyo kwenda mimi naomba serikali iweze kutatua tatizo la upatikanaji wa madawa kwenye vituo vyetu vya afya na zahanati”Alisema Mzee James Magazi.
“Pamoja na kwamba tumepatiwa vitambulisho vya matibabu lakini naona bado tatizo lipokubwa sana kwani hatupewi kipaumbele kwenye sekta ya matibabu”Alisema Ramadhani Shaban.
Kutokana na kero ambayo wameizungumza wazee ,mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye zoezi hilo,ametoa wito kwa viongozi wote wa vitongoji,vijiji na kata kuweka utaratibu wa dirisha la wazee na kupatiwa nafasi ya kwanza ya kusikilizwa na kutibiwa.
“Natoa wito kwa viongozi wa vijiji ,vitongoji,mitaa na kata kuakikisha
wanafatilia kwa makini zaidi swala la huduma kwa wazee kwa kuwapatia vitambulisho na pia zoezi la kupiga picha na kuwaandikisha wazee lifanyike kwa wazee wote”Alisema Kapufi
Awali akisoma taarifa ya zoezi hilo,afsa ustawi wa jamii,Shani Sanga
ameelezea tangu kuanza kwa zoezi hilo la vitambulisho vya msamaa wa
matibabu jumla ya wazee elfu kumi na sita (16000)wamekwisha kupigwa picha na kazi ya kutengeneza vitambulisho inaendelea kwenye ofisi ya mganga mkuu
wa halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment