Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran
nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi (katikati) akishirikiana na Kaimu Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu kukata
utepe kuashiria uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi
katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es
Salaam
Balozi
wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi
(kushoto) akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la
maonyesho la Bodi ya Filamu Tanzania wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki
ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya
Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu
Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu
(wapili kushoto) akiangalia moja ya kitabu kilichofanyiwa marekebisho na
wataalamu kutoka Iran baada ya kuchakaa wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya
wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba
ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji BASATA Bw.
Godfrey Mngereza
Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu
(Wanne kulia) akiangalia bidhaa za kiutamaduni za Iran zinazotengenezwa na malighafi
za shaba, fedha na dhaabu kutoka kwa Bw. Anmad Hamidi (kulia) wakati wa
uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam. Watatu
kulia ni Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe.
Mussa Far’hanqi
Kikundi cha
kiutamaduni kutoka Iran kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki
ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya
Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam.
Kikundi
cha ngoma kiitwacho Jivunie Tanzania Sanaa Group kikitumbuiza wakati wa
uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya washiriki wa maonyesho ya maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi
wakifuatilia matukio yaliyokua yakiendelea katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa
na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam
Watoto
wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran wakiimba wimbo wa taifa wa Iran wakati wa
uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu
(katikati) akifuatilia maonyesho yaliyokua yakiendelea wakati wa uzinduzi wa
maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya
Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa
Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi na
kulia ni Mkurugnzi Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw. Achiles Bufure
Balozi
wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi
(kulia) akizungumza na watu walioshiriki katika maonyesho ya maadhimisho ya
wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba
ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu
(kushoto mwenye sahani) akiongoza watu walioshiriki katika maonyesho ya
maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi katika Ukumbi wa Makumbusho ya
Taifa na Nyumba ya Utamaduni kuonja chakula cha watu wa Jamhuri ya Kiislam ya
Watu wa Iran leo Jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mhe.
Mussa Far’hanqi
Wadau wa utamaduni nchini wametakiwa kutumia
maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi kuenzi, kuendeleza na kudumisha
ushirikiano wa kiutamaduni katika tasnia ya Lugha, Sanaa, Filamu, Mila na
Desturi za Tanzania na Iran.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu wakati wa uzinduzi wa
maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi leo Jijini Dar es Salaam katika
Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni.
“Uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Iran ulianza
tangu karne ya 18 kipindi cha majilio ya wahenga wa kishirazi kutoka uajemi
ulioacha turathi za kiutamaduni za pande zote mbili” amesema Bw. Ryatuu.
Aidha, Bw. Ryatuu ameushukuru uongozi na watumishi
wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni katika kufanikisha sherehe hii
adhimu ya wiki ya utamaduni wa Washirazi.
Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Watu
wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mussa Far’hanqi ameushukuru uongozi wa Tanzania
kuendeleza na kuthamini utamaduni wa washirazi unaounganisha nchi ya Iran na
Tanzania.
Washirazi walikuja nchini tangu karne ya 18 kufanya
biashara katika Pwani ya Bahari ya Hindi na mji wao wa kwanza kufika ulikua ni
Kilwa mji ambao uliweza kustawi kiuchumi na kuweza kujitengenezea fedha zake
yenyewe na kufanya biashara na miji yote ya Pwani ya Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment