Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt.
John Pombe Magufuli ametoa wito kwa vyombo vya ulinzi kuendeleza vita dhidi ya biashara
haramu ya dawa za kulevya nchini.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar es
salaam wakati wa hafla ya kuwaapisha
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo na
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali James Aloyce Mwakibolwa.
Rais amesema kuwa kitendo cha Mkuu wa Jeshi la
Polisi Ernest Mangu kuwasimamisha baadhi ya watendaji kazi wake kimeipa heshima
jeshi la polisi nchini.
“Madawa ya Kulevya yanapoteza nguvu kazi za
watanzania hasa vijana, hivyo hii kazi si ya mtu mmoja ni ya wanzania wote
kushirikiana kwa pamoja katika kupambana na jambo hili kwa manufaa ya nchi”
alifafanua Rais Magufuli.
Mbali na hayo alisema kuwa, katika mapambano vipo
vikwazo kadha vitakavyojitokeza hivyo watanzania wanabudi kuungana kwa pamoja
dhidi ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya.
Katika hatua hiyo Rais Magufuli alisema kuwa kwa sasa
nchi inavyoelekea katika uchumi wa kati kupitia viwanda, amelitaka Jeshi la
Ulinzi nchini kusimamia na kujenga nchi ya viwanda kwa vitendo.
“haiwezekana Tanzania ya leo bado inaagiza sare
kutoka china,wakati nchi yetu ina wakulima wazuri wa pamba, hivyo vyombo vya
ulinzi mnatakiwa kujipanga katika hili, mkiamuua kuzungumza na baadhi ya
viwanda na kuwapa vipimo na ubora wa nguo, rangi watatengeneza. ”alisema Rais
Magufuli.
Alisema kuwa si kila kitu lazima kununua kutoka nje,
ni lazima kujipanga kwa kuhakikisha dhana ya viwanda inaanzia jeshini.
“Tubadilike tutengeneze Tanzania kwanza, maslahi ya
nchi yapewe kipaumbele, rasilimali zilizopo zitumike kwa manufaa ya nchi”
alisisitiza Rais Magufuli.
Katika hatua hiyo Rais Magufuli alitoa wito kwa
majeshi nchini kutoa ushirikiano kwa wateule, kwa kuhakikisha wanafanya kazi
kwa manufaa ya nchi na askari wengine.
Kwa upande wake Rais wa Mapinduzi ya Zanzibar Dkt
Ali Shein alisema kuwa jeshi la Tanzania linasifa kubwa ndani na nje ya nchi
hivyo anaamini wateule wapya watafanya kazi hiyo kwa umahiri mkubwa.
Naye Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange alisema kuwa
katika kipindi cha uongozi wake, ajali ya milipuko ya mabomu yaliyotokea
Mbagala na Gongola mboto ndio kilikuwa kipindi kigumu kwake kwani watu waliumia
na mali za wananchi na za jeshi zilipotea.
Wakati huo Jenerali Mkuu wa Majeshi aliyeapishwa leo
Venance Mabeyo ameahidi kuendeleza na kuimarisha ulinzi wa taifa la Tanzania
pale ambapo Jenerali Mstaafu Mwamunyange alipoishia na kama ilivyo majukumu ya
jeshi kimsingi.
Rais Magufuli pia aliwaapisha Kamishina Jenerali wa
Magereza Dkt Juma Alli Malewa ambaye alikuwa Kamishina wa Sheria na Uendeshaji
wa Taifa la Magereza.
Wengine ni Balozi Paul Mella ambaye ataiwakilisha
nchi ya Tanzania nchini katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Balozi Samweli
William Shelukindo ambaye anakwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Ufaransa
pamoja na Nyakimura Mathias Mhoji ambaye amekuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa
Umma.
Naye Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu amemuapisha
Kamishina wa Polisi Robert Boaz Mikomangwa ambaye amekuwa Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai.
No comments:
Post a Comment