Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi.
Akizungumza kwenye Semina ya kuwajengea uwezo na
mbinu za kuwabaini Raia wa kigeni wanaoingia
nchini bila ya kuwa na utaratibu afisa uhamiaji mkoani geita Wilfred Marwa amesema kuwa wageni
wengi ambao wamekuwa wakija
wamekuwa wakifika kwenye hotel na kuendelea kufanya mambo ambayo sio mazuri
katika mkoa wa Geita.
Akifungua semina hiyo ya siku moja mkuu wa wilaya ya
Geita mwl. Herman Kapufi amesema
kuwa kuna imani ambayo imejengeka
kwa wafanyabiashara kuwa kwa mtu ambaye
anakuwa na biashara nzuri na wateja wengi
kuhisiwa kuwa anatumia dawa za
kuvuta watu jambo ambalo ameeleza ni imani potofu.
Kwa upande wao washiriki kwenye semina
hiyo wameitaka idara ya uhamiaji kuwa na maadili yaliyo mema ikiwa
ni pamoja na kutoa vitambulisho pindi
wanapokuwa kwenye zoezi la ukaguzi lakini pia kutunza siri kwani wengi wao wamekuwa
wakiogopa kutoa ushirikiano kwa kuhofia
swala la usalama wao.
No comments:
Post a Comment