Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kuwataka viongozi wa majeshi nchini
kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote wa madawa ya kulevya bila
ya kujali nafasi zao, na umaarufu wao.
Akizungumza baada ya kuwaapisha Mkuu wa Majeshi nchini na
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Rais Magufuli amesema hakuna cha mtu maarufu wala mtoto
wa kiongozi, yeyote akikamatwa afikishwe mahakamani na kuagiza mahakama
kuharakisha kutoa hukumu zinazohusu dawa za kulevya.
Pia amesema hata kama ni mke
wake, naye anatajwa kuhusika na dawa za kulevya, akamatwe haraka na apelekwe
mahakamani.
"Hakuna cha mtu
Maarufu Mwanasiasa, Waziri, au Mtoto Wa Fulani hata mke wangu akijihusisha hapa
peleka maana madawa ya kulevya yamefikia pabaya" Amesema
Amesema vita hii asachiwe mtu
mmoja bali ni ya jamii nzima huku akifafanua umuhimu wa kuanza kukamata
watumiaji
"Hii vita si ya
Makonda peke yake bali ni ya watanzania wote, shika yeyote peleka
mahakamani na ndiyo maana nazungumza hakuna cha umaarufu, mkishika hawa wote
wanaovuta madawa ya kulevya wataeleza nani aliwauzia, na huyo aliyewauzia
ataeleza ameyapata wapi na huyo naye ukimshika ataeleza ameyapata wapi, lazima
mtengeneze hiyo chain yote ili kuhakikisha wote wanaohusika na madawa ya
kulevya wanashugulikiwa kikamilifu" alisema Rais Magufuli
Pia Rais Magufuli amekiri kuwa
anafahamu kuna watu walikuwa wanampigia simu IGP Ernest Mangu na kumpa ushauri
juu ya mambo ya madawa ya kulevya, hivyo Rais amesema kama angejaribu
kuwasikiliza basi leo asingekuwa na hiyo nafasi tena.
"Najua mtapata
vipingamizi fulani, nafahamu kuna watu walikupigia simu IGP kukushauri shauri
juu ya madawa ya kulevya, nashukuru hukuwasikiliza, ungewasikiliza ningejua na
wewe unahusika, na leo usingekuwa IGP" alisema Rais Magufuli.
Kauli hii ya Rais Magufuli inakuja ikiwa ni siku chache
tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda atangaze vita dhidi ya watu
wanaohusika na dawa za kulevya akianza kwa kutaja majina yakiwemo ya askari na
ya wasanii maarufu wa muziki na filamu akiwemo Wema Sepetu, Chid Benz, Vanessa
Mde n.k.
Siku tatu baada ya Makonda
kuwataja watuhumiwa hao, IGP Ernest Mangu alichukua hatua ya kuwasimamisha
askari 12 waliotajwa na kuahidi kuchukua hatua zaidi, jambo ambalo
limepongezwa na Rais Magufuli na kumueleza kuwa endapo asingechukua hatua hiyo,
angejua kuwa na yeye anahusika.
No comments:
Post a Comment