Mkuu wa mkoa wa Geita,Meja Jenerali Ezekiel Kyunga,akitfungua kikao cha wadau wa pamba Mkoani Humo. |
Wajumbe wakifatilia kwa makini kikao Kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Bukombe Nicas Mayala |
Wajumbe wakiendelea na majadiliano |
Wakuu wa wilaya Mkoani Geita wakifatilia kikao. |
Afisa kilimo wilaya ya Bukombe Joseph Machibya akitoa maelezo namna ambavyo wameweza kupiga hatua kwenye kilimo cha pamba. |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akisikiliza kwa makini kile ambacho kilikuwa kinatolewa na mkuu wa mkoa wa Geita. |
Serikali mkoani Geita ,imesema
kuwa itahakikisha inaboresha zao la pamba kwa kutumia viadudu ambavyo
vitasaidia kunusuru pamba kwenye maeneo ya vijijini ambako wakulima wengi
wanaendelea kulima.
Akizungumza kwenye kikao
cha wadau wa zao la Pamba kilichofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Mkoa na
kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka Wilaya zote za mkoa wa
Geita wakiwemo Maafisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika pamoja na Wakuu wa Bodi
ya Pamba kanda ya ziwa,
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja
Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga,amesema kuwa pamoja na hali ya changamoto
ya ukame na mvua kunyesha kwa uchache bado wakulima wameitikia wito
na kulima hali ambayo kwa sasa inatia matumaini kutokana na pamba kuoto
vizuri vijijini.
“Huko vijijini wamaenza
kulalamika kutokana na upungufu wa viuadudu sasa na sisi hapa lazima tupate
uvumbuzi kwamba hili tatizo la viuadudu tunalipatia majibu sahihi ambayo
yatawasaidia wakulima wetu kule vijijini, wakulima wameitikia vizuri pamoja na
hali hii ya mvua ambazo sio kamilifu, mvua ni chache, mvua ni haba lakini
wakulima wameitikia” alibainisha mh kyunga
Kwa upande wao baadhi ya
wajumbe akiwemo Emily Kasagara Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa
wa Geita na Safari Mayala Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
wameelezea changamoto dhidi ya zao la pamba na kusema
kuwa.
“Kuna changamoto mbalimbali
zilizojitokeza kuhusiana na zao hli la pamba, moja ni kuwa wakulima wengi
walielekeza nguvu zaidi kwenye mazao ya chakula kipindi mvua zilipoanza
kunyesha na badala ya zao la pamba kwa hiyo ndio maana hata katika taarifa yetu
kile kilimo cha pamba kiliextend mpaka mwezi Januari kwa sababu mvua zilipoanza
kunyesha tu wakawa wamerash kulima mazao ya chakula lakini baadae sasa wakalima
zao letu la pamba ambalo limeenda mpaka Januari” alisema
Aidha katika msimu wa
mwaka 2016-2017 Mkoa ulilenga kulima jumla ya tani elfu sitini na saba na mbili
(67,002) zilizotarajiwa kutoa mavuno ya tani elfu tisini na tatu mia nne
thelathini na saba (93,437) lakini changamoto ya mvua za vuli
kutonyesha vizuri katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Geita imeweza kusababisha
malengo hayo kutokufikiwa.
No comments:
Post a Comment