Wednesday, 8 February 2017

PICHA: IRAN KUADHIMISHA WIKI YA UTAMADUNI KWA MAONYESHO KATIKA UKUM



Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bibi. Zamaradi Kawawa akizungumza wakati wa Mkutano baina ya waandishi wa habari, wawakilishi kutoka Kituo cha Utamduni cha Irani pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo jijini Dar es Salaam.Kituo cha utamaduni cha Iran kimeaandaa maonyesho ya utamaduni yatakayofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, kuanzia terehe 10 - 12 Februari kwa kuonyesha tamaduni kutoka Iran. Kutoka kulia Kutoka kushoto ni Msaidizi wa Kituo cha Utamaduni wa Iran nchini Tanzania Bibi. Fatma Ally, Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa Iran nchini Ali Bagheni na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hajjat Shani Kitogo.



Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hajjat Shani Kitogo (wa pili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonyesho ya Utamaduni wa Iran leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yanatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, kuanzia na terehe 10 - 12 Februari kwa kuonyesha tamaduni kutoka Iran. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bibi. Zamaradi Kawawa, Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa Iran nchini Ali Bagheni  na Msaidizi wa Kituo cha Utamaduni wa Iran nchini Tanzania Bibi. Fatma Ally.


Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa Iran nchini Ali Bagheni akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya utamaduni wa Iran inayotarajiwa kufanyika kuanazia tarehe 10 – 12 Februari leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Msaidizi wa Kituo cha Utamaduni wa Iran nchini Tanzania Bibi. Fatma Ally na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hajjat Shani Kitogo.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bibi. Zamaradi Kawawa akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Kituo cha Utamduni cha Iran walioambatana na wasanii kutoka Irani pamoja na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. 


No comments:

Post a Comment