Afisa
mawasiliano na umasishaji wa jamii la haika,Mihayo Bupamba akitoa maelekezo kwa
wajumbe wakati wa Mkutano huo.
Afisa
mawasiliano na umasishaji wa jamii la haika,Mihayo Bupamba,akitoa elimu kwa
wajumbe juu ya zoezi la utafiti.
Mkuu wa
Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akitoa takwimu za Ukimwi
zilivyo katika hapa nchini.
Wajumbe
wakifatilia Mkutano.
Mkuu wa
Mkoa wa Geita akiendelea kutoa maelezo.
Wananchi Mkoani Geita wametakiwa kutoa ushirikiano wa karibu kwa watafiti
wa viashiria na matokeo ya ukimwi kwa mwaka 2016 ambao watafika kwenye maeneo
12 ambayo yamepangwa kufanyiwa utafiti.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja jenerali Mstaafu Ezekiel
Kyunga wakati wa Mkutano wa wadau wa utafiti wa viashiria na matokeo ya
ukimwa ya mwaka 2016 uliofanyika kwenye ukumbi wa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa alisema kiwango cha maambukizi kuwa kwasasa maambukizi
yamepungua kwa asilimia mbili hali ambayo imesaidia kuhifanya Tanzania
kuonekana kuwa chini katika ukanda wa jangwa la sahara.
“Kiwango cha maambukizo ya VVU katika tafiti zilizopita kinaonekana
kupungua kutoka asilimia 7 mwaka 2003 mpaka asilimia 5.1 mwaka 2011. Taarifa
hii inaonyesha kuwa juhudi hizo za Serikali zimeiwezesha Tanzania kupunguza
kiwango cha maambukizo ya VVU kwa asilimia mbili na kuifanya Tanzania kuwa ni
miongoni mwa nchi zenye kiwango cha chini cha maambukizo kati ya nchi za kusini
mwa jangwa la Sahara ambapo nchini nyingi za ukanda huu zina kiwango cha
maambukizo cha zaidi ya asilimia 10”Alisema Kyunga
Kwa upande wake afisa mawasiliano na umasishaji wa jamii la haika,Mihayo
Bupamba ameelezea kuwa katika mikoa ambayo wamepita wamepata ushirikiano wa
mwitiko mkubwa kutoka kwa wananchi ambao walikuwa wakiwafikia kwaajili ya
shughuli ya upimaji.
“Kiukweli mikoa ambayo tumepita kwaajili ya zoezi hili tumepata
ushirikiano mkubwa sana changamoto hazikosekani tulikutana na changamoto baadhi
ya watu ambao walikuwa wameandikishwa kukosekana kwenye makazi yao kwa maana ya
kwamba wameama makazi"Alisema Bupamba.
Pamoja na hayo utafiti huo utasaidia kukusanya taarifa za
upatikanaji na utumiaji wa huduma zitolewazo katika kudhibiti maambukizo
ya VVU na Ukimwi na vile vya tabia hatarishi vinavyochangia maambukizo ya
VVU.
Utafiti wa namna hiyo ni wa awamu ya nne kufanyika nchini ,unaoangalia
zaidi maswala ya afya ambapo utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2003/2004,wa
pili ulifanyika 2007/2008 na utafiti wa tatu ulifanyika 2011/2012
No comments:
Post a Comment