Monday, 13 February 2017

WANANCHI WA KATORO MKOANI GEITA WAIOMBA SERIKALI KUWEKA UMEME KWA BAADHI YA MAENEO



Baadhi ya wananchi wa  mtaa wa afya katika mamlaka ya mji mdogo wa Katoro wilayani na mkoani Geita wameiomba Serikali kuweka  umeme katika eneo hilo kutokana na kuwepo kwa  nguzo ambazo zimekaa takribani miaka miwili pasipo kuwa na umeme .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti  baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema  kuwa  wanaiomba Serikali  kupitia shirika la umeme  Tanzania  (TANESCO)  kufunga umeme katika eneo hilo kutokana na  nguzo kuu zinazo safirisha umeme kutoka mjini  kakola hadi katoro kupita eneo hilo

Wananchi hao wamesema kitendo cha kukosa umeme katika mtaa huo kinapelekea kudhorota kwa shughuli za kimaendeleo  kwani umeme ni fursa  nzuri  kwani  unaweza  kusaidia vijana ambao  hawana ajira  kujiar kupitia nishati hiyo kwa kufuga kuku  hata pengine kuchaji simu 

aidha mwenekiti wa mtaa huo Bw.Masaga Misso amesema kuwa   kumekuwepo  na idadi kubwa ya  wananchi ambao wanafika  katika ofisi yake  na kutoa  malalamiko  kuhusiana na sula hilo.

Masaga misso amesema  amejitahidi kulifuatilia suala hilo katika ngazi mbalimabli za uongozi  lakini hakuna utekelezwaji wowote ambao  umefanyika mpaka sasa


Hata hivyo meneja wa shirika la umeme  Tanzania mkoa wa geita  Bw. Joachim Rueta amewataka wananchi katika eneo hilo kuwa wavulivu kwani suala hilo lipo njiani kukamilika .

No comments:

Post a Comment