Ofisi ya Taifa ya
Takwimu imepokea msaada wa pikipiki 14 zenye thamani ya shilingi milioni 66
kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya ukusanyaji takwimu sahihi kwenye baadhi ya
mikoa
Mwakilishi kutoka
Benki ya Dunia Bi.Nadia Belhaji Hassine alisema lengo la kukabidhi msaada huo
ni kuboresha kazi ya ukusanyaji takwimu mikoani hasa sehemu ambazo hazifikiwi
kwa usafiri wa gari.
Bi. Hassine amesema kutokana na kazi
inayofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kufanikisha ukusanyaji na
usambazaji wa takwimu mbalimbali ambazo zimekuwa na matokeo chanya taasisi hiyo
imeamua kutoa msaada huo ili kuimarisha utendaji wa taasisi hiyo uweze kuwa
bora zaidi.
Akizungumza kwenye
hafla ya makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya
Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema msaada huo utaboresha na
kukuza tasnia ya takwimu ili kuweza kupata taarifa muhimu kwa ajili ya
maendeleo ya nchi.
Dkt Chuwa alisema
msaada huo utarahisiha usafiri wa kutoka eneo moja la utafiti hadi lingine na
kuweza kusaidia katika upatikanaji wa taarifa muhimu za kitafiti.
Akipokea moja ya
pikipiki hizo Bw.Lugome Kalisto kutoka Ofisi ya Takwimu Mkoa wa Pwani
aliishukuru Benki ya Dunia kwa msaada wa pikipiki hizo kwani wamekuwa wakipata
shida ya usafiri katika ukusanyaji wa takwimu hasa maeneo ambayo usafiri wa
gari haufiki.
”Tumekuwa tukipata
shida katika ukusanyaji wa takwimu hasa maeneo ambayo hayafikiki kirahisi kwa
gari hali ambayo imekuwa ikifanya utendaji wetu kuwa duni.Alisema Bw. Kalisto.
No comments:
Post a Comment