Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel
Kyunga,akitazama nafaka kwenye soko la ccm Kata ya katoro.
Mkuu wa
Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,akitoa agizo la kuakikisha
chakula kinalindwa kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bukombe.
Mkuu wa Mkoani wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga
,amewaagiza wakuu wa wilaya wote kuhakikisha wanasimamia vyakula
vilivyopo ikiwan ni pamoja na kudhibiti uhuzwaji wa nafaka kwenye wilaya
na mikoa jirani.
Mh. Kyunga ametoa maagizo hayo wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea
maghala ya vyakula kwenye wilaya za Geita,Bukombe na Mbongwe lengo likiwa ni
kujionea hali ya chakula Mkoani humo
Amesema kuwa ni vyema kwa wakuu wa wilaya kudhibiti chakula
kilichopo ikiwa ni pamoja na kuwaelekeza wananchi kutunza mazao katika
kipindi hiki ambacho mvua zimekuwa ni za kusuasua
“Niwaombe wakuu wa wilaya zote
kuwa waangalifu na kukilinda chakula kilichopo ili Wilaya na Mikoa ya jirani
isije ikachukua na kutuacha hatuna tena chakula lazima hiki kilichopo kitunze
na kuhifadhiwa na muwahimize wananchi walime mazaa ambayo yanakubaliana na mvua
kidogo Mfano,Viazi Mtama na muhogo”Alisema Kyunga
Akisoma taarifa ya mazao na hali ilivyo kwasasa kwenye soko la kibiashara
Katibu wa wafanya Biashara Soko la CCM Kata ya Katoro, Charles Mlale alisema
kuwa Bei ya nafaka kwa mwaka huu imepanda zaidi ikilinganishwa na mwaka
jana kwani mwaka jana Gunia la mahindi walikuwa wanachukulia kiasi cha Sh. elfu
themanini kwa sasa imefika kiasi cha laki na ishirini
Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa wilaya
Mkuu wa wilaya ya Bukombe Josephat Maganga amemhakikishia Mkuu wa
Mkoa kufanyia kazi maagizo aliyoyatoa ikiwa ni pamoja na kuakikisha hakuna mtu
ambaye hatatoka mikoa ya jirani au wilaya kuja kununua mazao yaliyopo kwenye
wilaya wanazozisimamia .
No comments:
Post a Comment