Wakazi wa Geita wameiomba Serikali kutatua suala la uhaba wa vituo vya afya pamoja na
zahanati mkoani hapa kutokana na
jambo hilo kupigiwa kelele kila
kukicha lakini limeonekana kuwa kama tatizo
la kudumu kwa baadhi ya maeneo
mkoani hapa.
Wakizungumza baadhi ya wananchi mkoani hapa
wameiomba Serikali kusogeza huduma hiyo
katika mazingira husika ili kuepuka
msongamano uliokithiri katika
hospital teule ya mkoa wa geita
pamoja na kupunguza vifo visivyo
kuwa vya lazima kwasababu ya ukosefu wa vituo vya afya na zahanati
vijijini .
Kwa upande wake Katibu wa vijana wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) Ally Rajabu amesema kuwa serikali
inawajibu wa kushughulikia suala hilo kikamilifu, kama imeweza kupiga kampeni
ya madawati kwa kila kijiji na imefanikiwa kwa asilimia kubwa basi hata katika sekta ya afya inaweza kufanya hivyo ili kupunguza changamoto zinazo kabiri sekta
hiyo.
Hata hivyo Kata ya Buhalahala ni miongoni mwa kata iliyopo
katika halma shauri ya mji wa Geita na ina idadi kubwa ya wakazi lakini
haina kituo cha afya wala zahanati jambo ambalo linawafanya wakazi wa eneo hilo
kutembea kwa umbali mrefu kufika katika hospitali teule ya mkoa ili kupata
huduma.
Kwa upande wa Diwani wa eneo hilo Bw.Eliasi Mussa ambapo yeye amewataka wakazi katika kata hiyo
kuwa wavumilivu kwani suala hilo la ujenzi wa kituo cha afya liko mbioni
kukamilika kwani kwa sasa wanatafuta eneo ambalo lipo karibu na
mazingira ya watu ili kujenga ktuo cha
afya kwa lengo la kuondoa adha inayo wasumbua wananchi katika eneo
hilo.
No comments:
Post a Comment