Mtoto mmoja amefariki dunia baada ya kuzama katika
bwawa la maji lililopo mtaa wa njia
panda katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani na mkoani geita.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na moja
jioni ambapo mtu huyo alikuwa akioga
katika bwawa hilo akiwa na wenzake baada ya mda mfupi alipotea ghafla kutokana
na bwawa hilo kuwa na kina kirefu ndipo
baadhi ya wakazi katika eneo hilo walipo
jitokeza na kujaribu kumtafuta ndani ya bwawa hilo lakini hawakufanikiwa
kumuona , ndipo shughuli za kumtafuta mtu huyo zimeendelea tena mapema hii leo na mnamo majira ya saa sita
mchana mwili wa marehemu huyo
umefanikiwa kuonekana .
Akizungumza Mwenyekiti
wa mtaa huo Bw. Michael Chuma amemtaja aliyefariki dunia kuwa ni Kamugisha Budodi
mwenye umri wa miaka 14 mkazi wa kijiji cha mapinduzi wilayani chato na alikuwa
mwanafunzi wa darasa la tano katika
shule ya msingi mapinduzi .
Aidha amewata wazazi na walezi katika mamlaka ya mji mdogo
wa katoro kutowaruhusu watoto wenye umri
mdogo kuchota maji wala
kuoga katika eneo hilo kutokana na bwawa
hilo kuwa na kina kirefu pamoja na toze nzito kitu ambacho kina kuwa hatarishi
kwa watoto hao.
Kwa upande wa baadhi ya wakazi katika eneo hilo wameiomba Serikali
ya mtaa huo kuweka uzio katika eneo hilo kwa lengo la kuzuia watoto wenye umri
mdogo kuto tumia bwawa hilo.
No comments:
Post a Comment